@trtafrikasw: Bila shaka, maendeleo na mapinduzi ya teknolojia, hususani ujio wa 'Akili Mnemba' au akili bandia kama inavyojulikana na wengi, umeibua hisia tofauti. Kwa sasa, ujio wa teknolojia hii umeleta hofu kuu mpya, wengi wakiogopa kupoteza kazi zao wakati wengine wana wasiwasi kuwa Akili Mnemba ni tishio jipya kwa wanadamu. Hali kadhalika, kukita mizizi kwa teknolojia hii ya ajabu kunaibua mijadala kati ya wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yaani TEHAMA juu ya namna inavyoweza kuweka rehani kazi ambazo kawaida hufanywa na binadamu. #trtafrikaswahili #ai #akilimnemba #sora #openai #chatgpt