@wepesitv: UKWELI WOTE SABABU ZA VIJANA 170 KULUNA KUUAWA CONGO DR Kinshasa. Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inadaiwa kuwaua vijana 170 waliokamatwa kwa madai ya kuwa wanachama wa makundi yanayotekeleza uhalifu wa mjini maarufu kama “Kuluna.” Vyombo vya Habari vya ndani Congo vinawaonyesha vijana hao wakiwa wamefungwa pingu mikononi huku wakibubujikwa machozi wakati wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Sheria wa taifa hilo, Constant Mutamba. Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limeripoti kuwa mamlaka za usalama nchini humo zimewakamata watuhumiwa zaidi ya 1,400 wa uhalifu huku wakitajwa kuwa ni wanachama wa Kundi la Kuluna. Amnesty International pia imesema kuwa kati ya waliokamatwa wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 ambao wanadaiwa kutenda makosa ya uhalifu ikiwemo uvamizi wa makazi na mauaji ya raia. Shirika la Habari la Associated Press limeripoti kuwa vijana takriban 170 kati yao wameshahukumiwa adhabu ya kifo na tayari taarifa zinadai kuwa vijana hao wameshauawa kwa kupigwa risasi nchini humo. Vijana hao walikamatwa kupitia Opereshezi za usalama zilizofanyika eneo la Ndobo, Lingala kwa lengo la kuwakamata vijana hao kati ya Desemba zikiongozwa waziri, Mutamba zililenga kukomesha magenge ya wahalifu katika Mji wa Ndobo wenye wakazi zaidi ya milioni 15. Shirika la Habari Associated Press limeripoti kuwa vijana hao walihamishwa kwa makundi makundi kutoka katika Gereza lililoko Jijini Kinshasa kwenda katika gereza lililoko mafichoni na lenye ulinzi wa hali ya juu kwa ajili ya kwenda kuuawa. Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria nchini Congo, Mutamba, wafungwa 70 kati yao walisafirishwa siku ya Jumapili huku wengine 102 wakipelekwa katika gereza la Angenga lililopo Kaskazini mwa Jimbo la Mongala nchini humo. Mutamba alisema vijana wote wa Kuluna walikutwa na hatia ya kufanya uhalifu wa mijini ‘urban bandits’ na wana umri kati ya miaka 18 hadi 35, japo hakuweka wazi ni lini vijana hao watauawa. Baadhi ya raia wa Congo DR wamepongeza uamuzi huo kwa kile wanachosema itasaidia kupunguza hofu iliyoibuliwa na matukio ya vijana hao huku wengine wakihofia kuwa kutekelezwa kwa adhabu ya kifo dhidi ya vijana hao kuwa ni ukatili na uvunjaji wa haki za binadamu. “Tunakubaliana na uamuzi huu wa waziri wa Sheria kwa sababu unalenga kukomesha uhalifu maeneo ya mjini. Awali ilikuwa ikifika Saa 2:00 usiku tu hauwezi tena kutembea mtaani ukiwa huru kwa sababu ya kuhofia vijana wa kundi la Kuluna,” Mkazi wa Goma Mashariki, Fiston Kakule, aliieleza Associated Press. Espoir Muhinuka, ambaye ni Mwanaharakati wa Haki za Binadamu alionya kuwa kuuawa kwa vijana hao huenda kukakiuka msingi wa utoaji wa haki na kuzitaka mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuheshimu haki za binadamu. Mwanaharakati huyo alisem anahofia kuwa huenda msukumo wa kisiasa ukasababisha uvunjaji wa haki na kusababisha watu kushtakiwa kisha kuuawa bila kufuata mfumo halali wa utoaji haki nchini humo. “Hali inayoendelea nchini Congo DR inachanganya na inahitaji Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati. Mapambano dhidi ya makundi ya uhalifu ya Mjini yanapaswa kwenda sawia na kuondoa Umaskini, ukosefu wa ajira na utengano wa jamii ambao wote unachangia kuibuka kwa makundi haya,” alisema mwanaharakati huyo. Congo ilifuta hukumu ya kifo mwaka 1981, kisha kuirejesha mwaka 2006. Mauaji ya mwisho kutokana na hukumu hiyo yalitekelezwa mwaka 2003. Machi 2024, Serikali ya Congo, ilitangaza utekelezwaji wa adhabu hiyo kwa watu wlaiotiwa hatiani kwa makosa makubwa ya uhalifu ikiwemo Uhaini. Mwezi Mei 2024, wanajeshi nane wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walitiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kifo na Julai 2024, wanajedhi wengine 25 nao walitiwa hatiani kwa kosa la aina hiyo japo wote hawafahamiki waliko hadi sasa na haifahamiki iwapo wameshauawa ama la.

WEPESI TV
WEPESI TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 14 January 2025 15:56:42 GMT
368769
3990
401
336

Music

Download

Comments

lameckfrank
lameckfrank :
I have a feeling that boy crying is very innocent
2025-01-16 13:39:35
65
sollyjacobs2
solly jacobs :
America is coming for the Congo
2025-01-17 21:00:36
4
ronnie.honalecki
Ronnie Honalecki :
never try this in Kenya 😏
2025-01-19 04:21:18
0
user7951132261983
samuel lb pln 2😉😆😆🥺🥺🤯 :
so young 😂😂
2025-01-16 04:36:26
7
nasianavillian
empress :
that president 🥺dont you even fear God
2025-01-17 04:39:50
7
sudykova2
sudykova2 :
maybe they could be given second chance
2025-01-15 21:00:07
13
shallom8precious
Isabwa Dee🙏 Catholic 💕 Girl :
not all are guilty akii may God comfort the innocent. I can c another is praying 💔
2025-01-17 07:06:27
5
mdawida.tiki3
mrembo wa taita :
keep the ten comandmants
2025-01-16 09:40:33
4
rachiemuradzi
Rachie Muradzi :
i don't no what they did why don't you give them second chance ummmmm
2025-01-16 21:41:49
2
noel.masavir
noel omondi apolo :
only God he's a judge
2025-01-15 15:25:50
22
shakilazuwena8
#First Daughter8 :
the others crying too bitterly looking innocent 😭
2025-01-16 20:09:53
5
ramadhani.omary04
Ramadhani Omary :
rip
2025-01-16 08:47:07
1
sbura275
sbura :
Plz explain president to say
2025-01-16 12:09:14
0
amstillruth3
Ruth Kamene :
ooh God😭😭
2025-01-17 10:44:16
0
keepkech2
Keepkech :
When is UN?
2025-01-17 12:31:24
0
lissafaith4
LISSA Faith :
😭 painful
2025-01-15 20:13:49
0
jacklinemgata
Jackie🦋🦋 :
so sad😭
2025-01-16 09:38:08
0
respect.makaranga
Respect Makaranga :
It's painful
2025-01-18 08:45:13
0
saniwier1
Saniwier :
duuuh so sad😭😭😭😭
2025-01-17 22:33:36
0
user442774041276
user442774041276 :
This is not good
2025-01-17 07:17:49
2
janesolomon681
Jane Solomon :
they are song young ak
2025-01-18 13:12:16
0
luizdiaz0007
italianofoca :
we watch and we don't judge 😭😭
2025-01-16 13:20:21
0
sarumanthewhite2
saruman thewhite :
so young😳
2025-01-15 20:50:35
0
reeen057
Maureenshishi :
proud to be a Kenyan
2025-01-17 07:42:57
0
user9132436852986
Didi :
Oh God they still young 😭😭😭
2025-01-17 07:54:37
0
To see more videos from user @wepesitv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About