@oscar_mkatoliki: KUPALIZWA BIKIRA MARIA MBINGUNI ( 15 AGOSTI ) Leo hii Kanisa linafurahia kutukuka kwake mtumishi mnyenyekevu wa Bwana. Ni sikukuu kubwa kupita zote zinazoadhimishwa na Kanisa kwa heshima yake. Kanisa Katoliki hufundisha kwamba Bikira Maria ambaye alihusiana kwa karibu sana na Kristo Mwanae katika mafumbo ya wokovu, alipalizwa mbinguni roho na mwili, na sasa hushiriki ushindi na heri yake. Tangu karne ya Tano, Wakristo wamesadiki kabisa kwamba mwili wake Bikira haukuoza kaburini, na Sikukuu ya Kupalizwa kwake imesherehekewa tangu karne ya sita. Mnamo mwaka 1950, Papa Pius wa Kumi na Mbili baada ya kuwahakikishia Maaskofu wa Kanisa zima, alitangaza kwamba fundisho hilo ni moja ya mafundisho makuu ya Imani Katoliki. Fundisho hili hutueleza kwamba hatuna budi kuuthamini mwili wa kibinadamu ambao baada ya ubatizo ni Hekalu la Roho Mtakatifu, na mwisho wa nyakati utafufuliwa kaburini. Ndipo wakombolewa wote watakuwa wanaishiriki, mwili na roho, heri ya mbinguni. Bikira Maria amewatangulia na kuishiriki sasa hali hiyo ambayo tumetayarishiwa sisi sote. Papa, wakati ule alipotangaza rasmi fundisho hilo, aliandika: "Ufufuko wa Bwana wetu ulikuwa utukufu wa ajabu na tukio lenye kusababisha ushindi mkuu juu ya dhambi na mauti; na Bikira Maria aliyeshiriki mapigano hayo, lazima ashiriki ushindi huo katika kutukuka kwa mwili wake wa Kibikira". BIKIRA MARIA MALKIA WA MBINGU, UTUOMBEE. #catholic #oscar_mkatoliki #tiktoktanzania🇹🇿 @Radio Maria Tanzania @Fr James Anyaegbu#tiktokpriest
Oscar Mkatoliki.
Region: TZ
Friday 15 August 2025 13:20:06 GMT
Music
Download
Comments
caramel_sabby💙✝️ :
Ahsante kwako pia uncle🥰😇
2025-08-16 17:23:38
4
Ney :
Maria Mtakatifu utuombee🙏🙏⛪
2025-08-15 13:39:28
2
Lucy maish :
Maria Mtakatifu Utuombee
2025-08-21 18:10:53
0
catholic_song :
Mama Maria, Utuombee 🙏🙏🙏
2025-08-15 13:32:49
5
Emily ggp :
catholic for life
2025-08-15 13:27:29
2
isojick :
asant kwako pia
2025-08-15 13:30:39
2
Jackson Bamfu :
Woooow Raha sanaaaa
2025-08-16 08:20:33
1
Gloria glory :
asnt na ww pia
2025-08-15 13:31:27
3
Bernadetha :
asnte Mwanangu mtumishi Mdogo🙏
2025-08-19 19:34:30
0
nanj :
Mama wetu tuombee🙏
2025-08-15 18:47:41
1
blandin_johnson :
heri kwako pia
2025-08-15 13:59:20
1
Pendo Roman :
kwak pia
2025-08-15 13:26:05
3
Teddy Francis :
Mam Maria mtakatifu utuombe wanao tu nakuomba mama yetu🙏
2025-08-15 14:02:17
1
Mar :
mama maria mama wa wote
2025-08-15 13:53:02
1
Gracious 27 :
mama mtakatifu utuombee🙏
2025-08-15 14:23:59
1
Ɓĺåč̣ķx̌x̌x̌ :
Maria Mtakatifu utuombee
2025-08-15 15:18:55
1
Emiliana 💕💕💕 :
mama Maria ni msaada wetu sote
2025-08-15 15:34:58
1
Constance Pretty Pretty :
mama Maria mtakatifu utuombee
2025-08-15 14:57:43
1
Rehema Mwinuka :
yaan sina neno zuri zaid,yakisema ubarikiwe unanikumbusha enzi nzur
2025-08-15 20:48:18
1
Imma❣️❣️❣️ :
Ahsanteeh kwakoo piah broo
2025-08-24 10:50:33
0
user8021318333749 :
Ubarikiwe kaka yangu.
2025-08-20 20:05:47
1
Anne Thuku :
kupalizwa???
2025-08-19 17:06:21
0
user87520312682414. rashaela :
fikisha salayangu eemama nariya
2025-08-19 04:14:29
1
Adele kamabu god is good :
mungu akubariki kakagu
2025-08-19 20:48:36
0
Romana Simon :
Maria mama wa mungu utuombeee kwa mwanao
2025-08-15 16:26:53
2
To see more videos from user @oscar_mkatoliki, please go to the Tikwm
homepage.