@ustadh101: 𝗜𝗙𝗔𝗛𝗔𝗠𝗨 𝗦𝗪𝗔𝗟𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗣𝗔𝗧𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗪𝗘𝗭𝗜/𝗝𝗨𝗔 Kila sifa njema anastahiki Allah Mlezi wa Viumbe wote, Sala na salam za Allah zimfikie Mtume Muhammad, Maswahaba na Jamaa zake wote na wale walio wafata kwa wema hadi Siku ya Qiyaama. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Kesho kutatokea Kupatwa kwa Mwezi, katika Makala hii fupi nitaelezea Hukumu mbali mbali za Kisharia kuhusu jambo hili la kupatwa Mwezi/Jua. Zifuatazo ni Hukumu mbali mbali zinazo husu Jambo hili:- 1. KUPATWA KWA MWEZI/JUA NI VITISHO VYA ALLAAH •Kupata kwa Jua/Mwezi ni miongoni mwa Vitisho vya Allah kwa waja wake katika kuwakumbusha kuacha Maasi na kurudi katika kumcha Allah. 2. SWALA YA KUSUFI •Swala ya Khusufi ni Swala ya Rakaa mbili yenye Visimamo viwili na Rukuu mbili kunapo tokea Kupatwa kwa Jua au Mwezi. 3. HUKUMU YA SWALA YA KUSUFI •Swala ya Kusufi ni Faradhi Kifaya, wakiitekeleza baadhi ya Waislamu wajibu wake unakuwa umedondoka kwa wengine. 4. MUDA WA SWALA YA KUSUFI •Muda wa Swala ya Kusufi ni Kuanzia kupatwa kwa Jua/Mwezi hadi hali itapo rudi kawaida. 5. NAMNA YA KUSWILI SWALA KUSUFI •Swala ya Kusufi inaswaliwa kama ifuatavyo :- (i) Kutia Niyah (moyoni) na Kuhirimia (ii) Kusoma Dua ya Ufunguzi wa Swala na Istiaadha. (iii) Kusoma Surat Al-Fatiha. (iv) Kusoma Sura ndefu baada ya Surat Al-Fatiha. (v) Kurukuu kwa muda mrefu unao karibiana na Kisimamo. (vi) Kuitidali na Kusoma Surat Al-Fatiha na Sura nyingine ndefu inayo karibia kisomo cha mwanzo. (vii) Kurukuu na kurefusha Rukuu kisha kuitidali, Kisha kusujudu na kurefusha Sujuudu. •Hadi hapa inakuwa imekamilika Rakaa ya Kwanza, Rakaa ya pili utafanya kama ulivyo fanya katika Raaka ya Kwanza, ispokuwa huta soma Dua ya Ufunguzi wa Swala wala Istiaadha. ZINGATIA :- •Swala ya Kusufi ina rakaa mbili na kila rakaa ina rukuu mbili na visimamo viwili. •Swala hii inaswaliwa kwa Sauti (Kisomo cha Qur'an) hata kama inaswaliwa Mchana. •Ni Sunna kwa Imaam kutoa Khutba fupi ambayo atahimiza watu kutubia kwa Allah kufanya Ibaada na Kumtii na kuacha Maasi na kukithirisha kufanya Toba na Dua na kuhimiza kutoa Sadaka na kuwataahadharisha kuhusu ubaya wa Maasi. •Swala hii huiswali hadi kutokee huko kupatwa Jua/Mwezi ama Taarifa tu kuwa Mwezi utakamatwa au Jua si Kigezo cha Kisharia pekee ya Kutekeleza Ibaada hii, bali hadi Tukio hilo lionkane kwa Macho. •Ikiwa Swala imeisha na bado Jua/Mwezi umepatwa muislamu ataendelea kufanya Dua na kuomba Msamaha na Toba. Allah atusamehe na Atufutie Madhambi yetu. Ameen وصلى الله وسلم وبارك على نبينا محمد وعلى آله وصحبه أجمعين . #swalatukusuf #viral_video #rwandatiktok #viral_video #rwandatiktok
ustadh101
Region: TZ
Sunday 07 September 2025 17:21:30 GMT
Music
Download
Comments
Mshirazi Mbuli :
ndo kwanza nimeswali leo tangu mizaliwe😭😭😭
2025-09-07 19:36:26
84
humairah djumaah 🦋🦋001 :
khusun khatimah yaa rabbi iyi ni dalili za kiama tufanye mema waislam wenzangu
2025-09-07 20:01:48
70
Slyme 💫 :
Sema uislamu umenyooka sana..Alhamdulillah
2025-09-07 19:39:07
46
tatu hamisi :
Emola wetu tusamee sisiwaja wako
2025-09-07 21:55:17
32
👑 baby huu♥️✌️ :
2namshukuru mungu kwa kila jambo hakika yeye ndio muweza kwa kila hatua 🙏
2025-09-07 21:19:49
20
israah cute :
tujitahd kufny ibada waislam wenzang
2025-09-07 19:59:36
18
jasmin_sweetcake :
ALLAHUMA AMEEN 🤲
2025-09-07 18:54:53
23
Iam_asnaty :
alhamdulilah
2025-09-07 20:32:22
9
Da rey :
ameen,, shukran kwa kutoa darsa,, ambao hawajui wamepata ufaham,, 🤲🤲
2025-09-07 19:47:57
21
madam626 :
aamin🙏
yarab asante kwa kutufanyia wepesi inshaallah 🙏🙏
2025-09-07 20:13:46
7
Lucky Girl :
Allah aqbar laillah illah Muhammad rasulullah 🤲🥹
2025-09-07 19:08:39
17
rahma hamissss :
mungu atujalie
2025-09-07 21:08:15
9
@____Mr____24 :
ameeen🤲🤲🤲🤲🤲🤲🤲
2025-09-08 03:53:32
7
Mwajuma Kassimu :
mungu atusamee kwamakosa yetu
2025-09-08 05:44:40
5
mishi love 🇰🇪🇴🇲 :
Allah atujalie mwisho mwema 🤲🤲🤲
2025-09-08 03:11:07
5
bisuraty💞saidy❤️ :
allah atupemwisho mwema ishaallah
2025-09-07 21:34:46
10
kisauti19 :
Allh aqbal
2025-09-07 19:48:53
5
🌸🌸sabrieshy❤💍🔐 :
amina🙏
2025-09-07 20:02:54
5
Banger_strawberry :
Ameen Yarabbi
2025-09-07 19:21:35
11
One the world 🌎 💙 :
Allah huma AMEIN
2025-09-07 19:14:28
5
SAP_🍁👑 :
Allahumma ameen
2025-09-07 19:52:45
5
Ukhty-muney 🦋🌸💫 :
Amiin yarabbi 🤲
2025-09-07 19:18:02
5
❤S@shul Hynny🦋 :
Allahuma Ameen
2025-09-07 18:12:37
9
Mwajabu :
thumaa ameen
2025-09-07 19:30:09
6
Alim k Simba🇺🇬🇹🇿💯💪 :
Allah Akbar 🙏🙏🙏❤️❤️❤️
2025-09-08 13:25:09
1
To see more videos from user @ustadh101, please go to the Tikwm
homepage.