@nurunaimani: Surah Hud || Ayah 9-11 Quran inamwangalia mtu kulingana na itikadi yake na tabia yake; kile anachokiamini na kile anachokifanya. Mtu anahukumiwa kuwa ni mwema pale anapokuwa mwema na anahukumiwa kuwa ni mwovu pale anapokuwa mwovu. Kwa hiyo anapoambiwa mtu ni kafiri ni kutokana na vile alivyo kwa mwendo wake na tabia zake alizojifunza; sio kuwa mtu ameumbwa hivyo. Ndio maana akawavua Mwenyezi Mungu wenye subira, akasema: isipokuwa wale waliosubiri; kama ambavyo mahali pengine mtu anazungumziwa kwa heshima; kama vile katika (17:70). Vinginevyo ingelikuwa kuadhibiwa ni dhulma. #nurunaimani #quran #nuruyetu #quranrecitation #dailyreminder