@neer.or.far: Fifth times the charm ✨🥲 #sprainedankle

Neer
Neer
Open In TikTok:
Region: US
Tuesday 30 September 2025 04:21:49 GMT
3641
88
3
0

Music

Download

Comments

swaytotheswe
swaytotheswe :
Omg spraining 5 times is cRAZY
2025-10-03 16:14:11
2
neer.or.far
Neer :
Uneven pavement will forever be my enemy 😭
2025-10-01 03:16:12
0
To see more videos from user @neer.or.far, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Martin Luther alikuwa mwanatheolojia wa Kijerumani na padre wa Kanisa Katoliki ambaye alizaliwa tarehe 10 Novemba 1483 katika mji wa Eisleben. Alikulia katika familia ya kawaida ambapo baba yake alitaka awe mwanasheria. Hata hivyo, maisha yake yalibadilika ghafla baada ya tukio la dhoruba kali lililomfanya aape kuwa atajiunga na maisha ya kitume iwapo angeokoka. Baada ya hapo aliingia katika utawa na kuwa mtawa wa shirika la Augustino. Katika maisha yake ya mwanzo ya kidini, Martin Luther alijulikana kwa nidhamu kali na jitihada za kujitakasa. Alijitahidi sana kufuata sheria za kanisa na kufanya ibada nyingi ili kupata wokovu Baadaye alipelekwa kusoma na kufundisha katika Chuo Kikuu cha Wittenberg, ambapo alijikita katika masomo ya theolojia. Hapa ndipo alianza kuchunguza kwa undani maandiko ya Biblia, hasa kitabu cha Warumi. Katika tafakari zake kwenye maandiko, aligundua kwamba wokovu haupatikani kwa matendo ya kibinadamu bali kwa imani tu. Wazo hili lilikuwa kinyume na mafundisho ya wakati huo ya Kanisa Katoliki. Katika kipindi hicho, Kanisa Katoliki lilikuwa likihusishwa na vitendo vya kuuza rehema (indulgences), ambavyo vilidaiwa kuwa vinaweza kupunguza adhabu ya dhambi. Mmoja wa wahubiri waliokuwa wakishadadia biashara hii alikuwa Johann Tetzel. Tetzel alihamasisha watu kununua hati hizi kwa ahadi ya kuwakomboa wao au ndugu zao kutoka mateso ya toharani (mahali kwa wafu). Hali hii ilimkera sana Martin Luther kwa sababu aliona kuwa ilikuwa ni upotoshaji wa mafundisho ya Kikristo. Mnamo tarehe 31 Oktoba 1517, Martin Luther alichukua hatua ya kihistoria kwa kuandika hoja 95 zilizojulikana kama '95 Theses'.Aliweka hati hiyo kwenye mlango wa kanisa la All Saints' huko Wittenberg. Lengo lake halikuwa kuanzisha mgawanyiko bali kuchochea mjadala wa kitaaluma kuhusu matumizi mabaya ya vitubio au indulgences. Katika hoja zake 95 ,Luther alipinga waziwazi wazo kwamba rehema zinaweza kununuliwa kwa pesa. Alisisitiza kuwa toba ya kweli ni jambo la ndani ya moyo na haiwezi kubadilishwa na malipo ya kifedha. Pia alikosoa mamlaka ya papa katika kutoa msamaha wa dhambi, akisema kuwa ni Mungu pekee mwenye uwezo huo. Hoja zake zilisambaa kwa haraka sana kote Ulaya kutokana na uvumbuzi wa mashine ya uchapishaji nyaraka. Watu wengi walivutiwa na mawazo yake kwa sababu yalitoa changamoto kwa mfumo uliokuwa umezoeleka kwa muda mrefu. Hii ilisababisha mvutano mkubwa kati yake na viongozi wake wa Kanisa Katoliki. Kanisa lilijaribu kumzuia na kumtaka abadili msimamo wake, lakini Luther alikataa. Mwaka 1520, Papa Leo X alimtolea hati ya kumtaka ajirekebishe la sivyo atatengwa na kanisa. Luther aliichoma hadharani hati hiyo kama ishara ya kupinga mamlaka ya papa. Mwaka uliofuata, alihudhuria mkutano mbele ya Mfalme Charles V. Hapa aliombwa tena aondoe mafundisho yake, lakini alikataa akisema hawezi kukana dhamiri yake wala maandiko ya Biblia. Kauli yake maarufu ilikuwa kwamba
Martin Luther alikuwa mwanatheolojia wa Kijerumani na padre wa Kanisa Katoliki ambaye alizaliwa tarehe 10 Novemba 1483 katika mji wa Eisleben. Alikulia katika familia ya kawaida ambapo baba yake alitaka awe mwanasheria. Hata hivyo, maisha yake yalibadilika ghafla baada ya tukio la dhoruba kali lililomfanya aape kuwa atajiunga na maisha ya kitume iwapo angeokoka. Baada ya hapo aliingia katika utawa na kuwa mtawa wa shirika la Augustino. Katika maisha yake ya mwanzo ya kidini, Martin Luther alijulikana kwa nidhamu kali na jitihada za kujitakasa. Alijitahidi sana kufuata sheria za kanisa na kufanya ibada nyingi ili kupata wokovu Baadaye alipelekwa kusoma na kufundisha katika Chuo Kikuu cha Wittenberg, ambapo alijikita katika masomo ya theolojia. Hapa ndipo alianza kuchunguza kwa undani maandiko ya Biblia, hasa kitabu cha Warumi. Katika tafakari zake kwenye maandiko, aligundua kwamba wokovu haupatikani kwa matendo ya kibinadamu bali kwa imani tu. Wazo hili lilikuwa kinyume na mafundisho ya wakati huo ya Kanisa Katoliki. Katika kipindi hicho, Kanisa Katoliki lilikuwa likihusishwa na vitendo vya kuuza rehema (indulgences), ambavyo vilidaiwa kuwa vinaweza kupunguza adhabu ya dhambi. Mmoja wa wahubiri waliokuwa wakishadadia biashara hii alikuwa Johann Tetzel. Tetzel alihamasisha watu kununua hati hizi kwa ahadi ya kuwakomboa wao au ndugu zao kutoka mateso ya toharani (mahali kwa wafu). Hali hii ilimkera sana Martin Luther kwa sababu aliona kuwa ilikuwa ni upotoshaji wa mafundisho ya Kikristo. Mnamo tarehe 31 Oktoba 1517, Martin Luther alichukua hatua ya kihistoria kwa kuandika hoja 95 zilizojulikana kama '95 Theses'.Aliweka hati hiyo kwenye mlango wa kanisa la All Saints' huko Wittenberg. Lengo lake halikuwa kuanzisha mgawanyiko bali kuchochea mjadala wa kitaaluma kuhusu matumizi mabaya ya vitubio au indulgences. Katika hoja zake 95 ,Luther alipinga waziwazi wazo kwamba rehema zinaweza kununuliwa kwa pesa. Alisisitiza kuwa toba ya kweli ni jambo la ndani ya moyo na haiwezi kubadilishwa na malipo ya kifedha. Pia alikosoa mamlaka ya papa katika kutoa msamaha wa dhambi, akisema kuwa ni Mungu pekee mwenye uwezo huo. Hoja zake zilisambaa kwa haraka sana kote Ulaya kutokana na uvumbuzi wa mashine ya uchapishaji nyaraka. Watu wengi walivutiwa na mawazo yake kwa sababu yalitoa changamoto kwa mfumo uliokuwa umezoeleka kwa muda mrefu. Hii ilisababisha mvutano mkubwa kati yake na viongozi wake wa Kanisa Katoliki. Kanisa lilijaribu kumzuia na kumtaka abadili msimamo wake, lakini Luther alikataa. Mwaka 1520, Papa Leo X alimtolea hati ya kumtaka ajirekebishe la sivyo atatengwa na kanisa. Luther aliichoma hadharani hati hiyo kama ishara ya kupinga mamlaka ya papa. Mwaka uliofuata, alihudhuria mkutano mbele ya Mfalme Charles V. Hapa aliombwa tena aondoe mafundisho yake, lakini alikataa akisema hawezi kukana dhamiri yake wala maandiko ya Biblia. Kauli yake maarufu ilikuwa kwamba "atasimama kwenye ukweli alioamini". Baada ya mkutano huo, alitangazwa kuwa mhalifu na alilazimika kujificha. Alipata hifadhi katika kasri la Wartburg ambapo alikaa kwa muda. Akiwa huko, alitafsiri Biblia ya Agano Jipya kutoka Kilatini kwenda Kijerumani, hatua iliyosaidia sana watu wa kawaida kuielewa Biblia kwa lugha yao. Tafsiri yake ya Biblia ilikuwa na matokeo makubwa sana kwa jamii ya Wajerumani. Iliimarisha matumizi ya lugha ya Kijerumani na kuwapa watu uwezo wa kusoma maandiko bila kutegemea viongozi wa dini pekee. Hii pia ilichochea zaidi mageuzi ya kidini yaliyokuja kujulikana kama Protestant Reformation. Katika mafundisho yake, Luther alisisitiza mambo makuu kama “imani pekee” (sola fide), “neema pekee” (sola gratia), na “maandiko pekee” (sola scriptura). Mbali na kazi yake ya kidini, Luther pia alioa mtawa wa zamani aitwaye Katharina von Bora. Martin Luther alifariki tarehe 18 Februari 1546 katika mji aliozaliwa wa Eisleben. Urithi wake unaendelea kuonekana hadi leo kupitia makanisa ya Kiprotestanti likiwemo Lutheran huko baadae.

About