@trtafrikasw: Katika Mkutano Mkuu wa 80 wa Umoja wa Mataifa uliomalizika wiki iliyopita kule mjini New York nchini Marekani, kilio kikubwa kilichoibuka kutoka kwa viongozi wa Afrika ilikuwa ni juu ya ukosefu wa uwakilishi wa bara katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama mwanachama wa kudumu. Kwa sasa, Baraza la Usalama tayari lina wanachama watano wa kudumu na Afrika inadai nafasi mbili . Hata hivyo jinsi ya kuchagua nchi hizo mbili huenda ikawa changamoto. #un #africa #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪 #ugandatiktok #swahilitiktok