@clevin.felcian: *MAISHA YA WATAKATIFU* *MT. YOHANE WA KAPISTRANO,* PADRE MFRANSISKO ( 23 OKTOBA ) Yohane alizaliwa Kapistrano (Italia) mwaka 1386. Alijifunza sheria huko Perugia, na kwa muda, alikuwa hakimu na pia aliwahi kuwa gavana wa Perugia. Huko aliyatekeleza mambo yote kwa hekima na uadilifu. Watu walimsifu sana. Miaka minne tu baada ya kufunga ndoa, yeye na mke wake walikubaliana kutengana. Yohane aliona kuwa anasa za dunia na furaha zake si kitu, akavutwa kujiunga na utawa wa Mt. Fransisko. Kifungo cha ndoa kilipokatwa kwa ruhusa rasmi, akakubaliwa kuingia utawani, na mwaka 1420, akapadirishwa. Utawani alionesha mfano wa kila fadhila, akisema daima: "Nimepata jina hili la Yohane ili nipate kuwa mfuasi mwaminifu wa Kristo na mtoto mpendwa wa Bikira Maria". Akaendelea katika kujikamilisha kiroho. Alijifunza sana Teolojia, akamchukua Mt. Bernardino wa Siena kama mwalimu wake mkuu. Alikuwa mhubiri hodari sana, alitembea mahali pengi, akifundisha na kuwaongoza watu. Alihubiri katika nchi ya Italia, Ufaransa, Ujerumani, Austria, Hungaria na Poland. Alijishughulisha pia katika harakati za kuleta mapinduzi katika Shirika la Mtakatifu Fransisko, kwani maisha yao ya kiroho yalikuwa yametetereka. Vile vile alipewa jukumu la kuwaimarisha Wakristo katika imani Katoliki, na kuwapinga wazushi wa siku zile. Baadaye, katika mwaka 1455, Waturuki Waislamu waliwashambulia Wakristo. Padre Yohane alihubiri vita vya msalaba dhidi yao, kwa ajili ya kuwaokoa Wakristo. Juhudi zake huko Bavaria (Ujerumani) na katika Austria mwaka 1456 hazikufaulu sana. Punde Waturuki wakaingia hata Belgrado (Yugoslavia). Padre Yohane alikazana zaidi kuhubiri ili Wakristo waunde jeshi, na kupigana dhidi ya hao Waturuki. Mwisho alikwenda vitani mwenyewe, akimfuata jemedari Hunyadi wa Hungaria, kusudi kuwatia moyo askari Wakristo katika mapigano. Basi, Wakristo waliuokoa mji wa Belgrado, na kisha wakawashinda Waturuki. Hivyo Ulaya ya Magharibi iliokolewa siku hizo. Baada ya vita, ulizuka ugonjwa kutokana na maiti nyingi zilizokuwa zimeachwa mijini bila kuzikwa. Padre Yohane alishikwa na ugonjwa huo, akafa tarehe 23 Oktoba mwaka 1456. Alitajwa kuwa Mtakatifu mwaka 1724. *MT. YOHANE WA KAPISTRANO, UTUOMBEE* *MASOMO YA MISA* I. Rum. 6:12-18 Zab. 124 INJILI: Lk. 12:39-48

Mimi ni Mkatoliki. 🇹🇿
Mimi ni Mkatoliki. 🇹🇿
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 22 October 2025 18:08:09 GMT
137
28
1
1

Music

Download

Comments

ibrahim.katolo1
Ibrahim katolo :
🙏🙏🙏🙏
2025-10-22 19:02:55
0
To see more videos from user @clevin.felcian, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About