@destiny_dreamfate: BOND FUND VS TREASURY BONDS 1. AINA YA UWEKEZAJI Bond fund ni moja kati ya mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa UTT AMIS ambao umeelekeza asilimia kubwa ya uwekezaji wake katika hatifungani za serikali wakati Treasury Bonds ni uwekezaji katika hatifungani za serikali unaohusisha kuikopesha pesa serikali. 2. Muda wa uwekezaji BOND FUND ni uwekezaji ambao hauna maturity period yani ni uwekezaji wa muda wowote na bila ukomo wa muda wa uwekezaji. Treasury Bonds Zina maturity period yani ukomo wa uwekezaji wa hadi miaka 25 na ukinunua moja hauwezi kuongezea hapo ila unaweza kununua Bond nyingi kwa kadri zitakavyokuwa zinatangazwa 3. KIANZIO Bond fund Ina vianzio aina tatu. Kianzio cha Tshs 50,000 hakuna gawio), 5 M unapata gawio mara la mbili kwa mwaka, 10 M unapata gawio kila mwezi. Treasury Bonds Zina kianzio cha Tshs 1 M na gawio ni mara 2 kwa mwaka yani kila baada ya miezi 6) na unanunua kulingana na calender ya mnada ya BOT 4. MANUNUZI Unaweza kununua au kuuza vipande vya mfuko wa kupitia application ya UTT AMIS, menu ya *150*82#, kuhamisha kutoka benki kujaza fomu na kupeleka ofsini kwao au kwa kupitia wakala wa CRDB Bank au kwa kufika katika tawi la CRDB Bank lililopo karibu nawe. Treasury Bonds itakubidi kununua kupitia kwa madalali wa Hisa (stock brokers) walioidhinishwa na CMSA. 5. AINA YA FAIDA BOND FUND inatoa faida kwa mfumo wa Riba limbikizi yani compounding interest wakati Treasury Bonds inatoa faida kwa mfumo wa Fixed interest inayoitwa Coupon rate 6. DHAMANA YA MKOPO Aina zote mbili za Uwekezaji zinaweza kutumika kama dhamana ya mkopo. #fyp #foryoupage #viral #tiktok #fyppppppppppppppppppppppp