@simulizinasauti: Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza kuhusu maandamano ya Oktoba 29, akiyataja kama vurugu zilizopangwa kuipindua serikali, na si mijadala ya kudai haki kama ilivyodaiwa na waandaaji wa maandamano hayo. Akizungumza kwenye mkutano na wazee wa Dar es Salaam, Rais Samia alikemea vikali wakosoaji wa hatua kali zilizochukuliwa na vyombo vya dola katika kukabiliana na maandamano hayo. Katika hotuba yake, Rais Samia alihoji: “Wengine wanasema nguvu kubwa ilitumika… walitaka iwe vipi? Nguvu inavyotumika inaenda Sawa na tukio lililopo! Nguvu ndogo ipi itumike? Tuwache wamalize walicholipwa kufanya?” Kwa kauli hiyo, rais alisisitiza kuwa serikali ilikuwa na wajibu wa kulinda amani, mali za umma, na uongozi wa nchi, akidai ushahidi wa ndani unaonesha baadhi ya vijana walilipwa ili kuchochea vurugu na kusababisha taharuki iliyoonekana mitaani. Kauli ya rais imeibua mjadala mpana mtandaoni na kwenye majukwaa ya siasa, huku wadadisi wakisema hotuba hiyo inaashiria kuwa serikali haiamini kuwa maandamano yalikuwa ya kawaida, bali mpango mpana wa kuvuruga utawala.
Simulizi na Sauti
Region: TZ
Tuesday 02 December 2025 11:03:08 GMT
Music
Download
Comments
Mambomaridhawa_Podcast :
sahihi kabisa
2026-05-07 14:46:27
0
Fey :
mmmh
2025-12-02 11:47:15
0
Man Rasheed :
😳😳😳
2025-12-02 11:26:37
0
To see more videos from user @simulizinasauti, please go to the Tikwm
homepage.