@pius_rubinda: Maelekezo: Mfwatiliaji wangu Haya ni maombi ya vita , unapo ya Fanya lolote laweza tokea hivyo usishangae Pili haya yawe maombi yako endelevu maana Kila siku ufalme wa Giza unaibuka kupambana na wewe hivo hakikisha na wewe Kila siku unapata nafasi ya kuvunja madhabahu inayo inuka juu yako maana biblia inasema _ Mathayo 13:25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Hivyo vita ya kiroho haushindi Leo ukatulia Bali Kila wakati unahakikisha moto wako hauzimi na huo ndio ushindi wako kiroho _ hakikisha moto wako katika kuomba maombi haya ya vita hauzimi Mwisho : Madhabahu za Giza zinavunjwa Kwa maombi ukiweza kuambatanisha sadaka inatia uzito ila _ sio Sheria maana Kuna wakati utaikosa hivyo ikiwa Roho wa Mungu anakuongoza kuambatanisha sadaka au kufanya lolote la zaidi katika maombi haya fanya maana yeye ndie mkuu katika eneo la ukombozi _ Luka 4:18