@pastorgeorgemukabwajrc: FAHAMU NGUVU ILIYO NDANI YA NENO LA MUNGU 📖🔥 Huwezi kumjua Mungu kwa undani pasipo kulijua Neno lake. Kiwango cha ufunuo wako wa Mungu kinaendana moja kwa moja na kiwango cha Neno ulilonalo ndani yako. Mungu hujifunua kupitia Neno, na hapo ndipo uhusiano wa kweli huanza. Mungu hukufungulia milango pale ulipopokea na kusimamia Neno lake. Lakini shetani hupata nafasi ya kukushambulia anapogundua hujui Neno kwa sababu ujinga wa Neno huacha mianya ya kiroho. Chochote utakachokiona katika Neno la Mungu, Yeye yuko tayari kukifunua na kukitimiza maishani mwako. Shikilia Neno. Ishi kwa Neno. Ndani ya Neno ndipo kuna nguvu, ulinzi, na mwelekeo wa maisha yako. 📖 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.” Zaburi 119:105 📺 Somo kamili linapatikana YouTube: Pastor George Mukabwa