@siasa.halisi: Baada ya Kambona kung'oa Pisi ya Kichaga pale London, Yeye na Mwalimu walirudi Bongo kwa ajili ya kufanya maandalizi ya makabidhiano ya uhuru wa Tanganyika. llipofika mwaka 1961, Walitimba kwenye ofisi za Gavana wa Uingereza na kufanya kikao kizito mno. Hawakutaka utani kabisa. Walikabia juu sana na kufanya "PRESINGI" kama Pacome, Ndipo Gavana akamchana Nyerere kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa uhuru. Usichokijua ni kwamba, kwenye upangaji wa tarehe ya kukabidhiwa kwa uhuru wa Tanganyika, Mara ya kwanza, Gavana alipanga kukabidhi Uhuru huo siku ya Disemba 28, 1961 Lakini mara baada ya kuwasiliana na Malkia Eliza (Mmiliki wa Tanganyika) Akaambiwa kwamba, kwa tarehe hiyo yeye hatakuwepo ofisini, Atakuwa "VAKASHENI" anakula Bata la Krismasi na Mwaka Mpya, Hivyo Gavana ikambidi arudishe siku nyuma na kuichagua 9 Disemba 1961, Kama tarehe rasmi ya kukabidhi uhuru wa Tanganyika. Hapo sasa ndipo mkeka wa Nyerere ulipoTIKI kwa 100% Kama ingekuwa ni dalili ya mvua, basi mawingu yalishona angani kwelikweli. Chapu kwa haraka, Gavana alifanya mabadiliko ya kiuongozi kwenye Serikali ya Tanganyika, Akampandisha cheo Nyerere kutoka kuwa Waziri Kiongozi, Hadi kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika. Nakumbuka alianza kukitumikia cheo hicho kwenye sherehe za kwanza za Mei Mosi, 1961. llipofika 9 Disemba 1961, Gavana alikabidhi uhuru wa Tanganyika kwa Mwl. Nyerere, Na hapo ndipo tukaanza kucheza YOPE Mwalimu hakulemba wala nini, Akamvuta mwanae (Oscar Kambona) na kumpa shavu la kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa kwanza wa Tanganyika. Cheo ambacho hakudumu nacho sana kwa maana ilipofika mwaka 1962, Alimteua kuwa Waziri wa Ulinzi na baadae Waziri wa Mambo ya Ndani. Cha ajabu sasa, eti Gen-Z wanabeza kwa kusema, Mwalimu alipewa uhuru kama Kashata. Kwamba hakuna alichofanya bali alipewa tu kama kikombe cha maji. Dadeki, mnaleta mzaha kwenye mambo ya KIUME. Endeleeni Kujidanganya, lakini kwenye mishe za kuutafuta UHURU wa Tanganyika, Kuna wanaume wengi walivuja sana jasho na KUFA, ili leo hii mpate uhuru wa kukomenti huo ujinga wenu. Unataka "MADINI" zaidi? Wacha kwanza nikatafute Maji ya KUOGA, Usiondoke, NAKUJA 🫵🏾 #tiktoktanzania🇹🇿 #tiktokkenya🇰🇪 #fypシ゚viral #trend #History

Siasa Halisi🌍
Siasa Halisi🌍
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 11 January 2026 10:42:05 GMT
4027
117
3
1

Music

Download

Comments

cynodon2009
cynodon2009 :
safii
2026-01-15 09:26:43
1
queen_wah22
Queen Wah :
🔥🔥👌
2026-01-12 07:33:16
1
tibloh360
Naloli :
🔥🔥🔥
2026-01-11 21:48:54
1
To see more videos from user @siasa.halisi, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About