@khajirath._tiba._: VIDONDA VYA TUMBO (Stomach Ulcers) Vidonda vya tumbo huanza pale ukuta wa ndani wa tumbo au utumbo mdogo unapochubuka/kupata jeraha kutokana na: • Asidi kali ya tumbo Maambukizi • Dawa au mtindo mbaya wa maisha Ukuta wa tumbo unaposhindwa kujilinda dhidi ya asidi, jeraha huanza polepole hadi kuwa kidonda. Sababu kuu za vidonda vya tumbo 1. Maambukizi ya bakteria H. pylori 2. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za maumivu (aspirin, ibuprofen, diclofenac n.k.) 3. Kunywa pombe kupita kiasi 4. Uvutaji wa sigara 5. Msongo wa mawazo (stress) wa muda mrefu 6. Kula vyakula vyenye pilipili nyingi, mafuta mengi au kula bila mpangilio 7. Kukosa kula kwa muda mrefu (tumbo tupu mara kwa mara) 8. Kurithi (historia ya familia kuwa na vidonda) *Dalili za vidonda vya tumbo* • Maumivu ya tumbo (hasa juu ya kitovu au chini ya kifua) • Maumivu yanayoongezeka ukiwa na tumbo tupu Kiungulia/kuchoma kifuani • Kichefuchefu au kutapika • Gesi nyingi tumboni • Tumbo kujaa haraka hata ukila kidogo • Kupungua uzito bila sababu Kinyesi cheusi au chenye damu (dalili hatari) Madhara ya vidonda vya tumbo Kama havitatibiwa mapema vinaweza kusababisha • Kutokwa damu tumboni • Upungufu wa damu (anemia) • Kupasuka kwa tumbo (perforation) - hatari sana • Kuziba kwa njia ya chakula • Maumivu sugu na kudhoofika kwa mwili • Hatari ya kifo kwa visa vikali *Hatua za kuchukua ukiwa na vidonda vya tumbo* 1. Fika hospitali mapema kwa vipimo (H. pylori, ultrasound au endoscopy) 2. Tumia dawa kwa usahihi kama ulivyoelekezwa (usikatize dozi) 3. Epuka pombe, sigara na kahawa 4. Punguza stress na usingizi wa kutosha 5. Kula kwa mpangilio - usiruke milo 6. Epuka vyakula vinavyochochea asidi (pilipili, mafuta mengi, soda) 7. Kunywa maji ya kutosha 8. Usitumie dawa za maumivu bila ushauri wa daktari Hitimisho Vidonda vya tumbo vinatibika kabisa kama vikigundulika mapema. Kupuuza dalili ni kujitafutia madhara makubwa. ✍️KAMA TAYARI UNA TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO WASILIANA NAMI SULUHISHO LIPO LA MOJA KWA MOJA 0683096968

khajirath _Tiba _lishe
khajirath _Tiba _lishe
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 12 January 2026 13:45:15 GMT
2454
16
1
16

Music

Download

Comments

ngebamedard
I RENE Samwely :
khiii!!! silious?
2026-03-17 13:13:21
0
To see more videos from user @khajirath._tiba._, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About