@berry_product_tanzani: *DALILI ZA KUKUJULISHA UNA TATIZO LA KIUNGULIA* *Dalili kuu ya matatizo haya ni kupatwa na kiungulia mara kwa mara ambapo huambatana na koo la chakula kuwaka moto pia maumivu ya kifua na hali hii huzidi zaidi pale mtu anapolala kichwa kimeinama.* *Kiungulia hiki huanza baada ya lisaa limoja na kuisha baada ya masaa mawili baada ya kula.* *Pia dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale mtoto anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula* *Dalili zingine ni kama;* *♻️Tumbo kuunguruma na* *Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.* *♻️Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali* *♻️Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula* *♻️Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka.* *♻️Mdomo kuwa mchachu muda mwingi* *♻️Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu* *♻️Mdomo kukauka* *♻️Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.* *♻️Tumbo kujaa gas baada ya kula*