@shamsharap: urban pipe slipper😍

𝒮𝒶𝓂𝒶𝓃𝓉𝒽𝒶💋
𝒮𝒶𝓂𝒶𝓃𝓉𝒽𝒶💋
Open In TikTok:
Region: PH
Friday 30 January 2026 17:01:03 GMT
336
1
0
1

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @shamsharap, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

🛑 HATUA (6) ZA KUJIONDOA KWENYE UHUSIANO UNAOKUCHANGANYA NA KUKUTESA BILA KUJILAUMU NA KUUMIA KIHISIA. __________________________________________________ Huenda bado unampenda, lakini umechoka kuishi kwenye mashaka. Leo anakupa matumaini, kesho anakupuuza. Unataka kuondoka, lakini moyo wako bado unasema, “Labda atabadilika.” Kujiondoa hakumaanishi kwamba hukumpenda. Inamaanisha umeamua kutokupoteza mwenyewe katika uhusiano unaokuumiza. 1️⃣ KUBALI HALI HALISI YA UHUSIANO. Acha kuangalia zaidi kile unachotamani kitokee. Angalia kinachotokea sasa. Jiulize: “Uhusiano huu unanipa amani au unanifanya niishi kwenye mashaka?” Usijenge uamuzi wako juu ya matumaini ya mtu kubadilika. 2️⃣ ACHA KUJILAUMU. Usijilaumu kwa kumpenda, kuamini au kuvumilia. Tambua makosa yako pale ulipokosea, jifunze, kisha songa mbele. Kujilaumu hakubadilishi yaliyopita; kujitambua kunakusaidia kufanya maamuzi bora yajayo. 3️⃣ TAFUTA UFAFANUZI Kama hujui uhusiano unaelekea wapi, zungumza kwa uwazi. Uliza unachohitaji kujua, kisha angalia kama majibu yake yanaendana na matendo yake. Usilazimike kuwa mpelelezi ili kujua nafasi yako katika maisha ya mtu. 4️⃣ WEKA MIPAKA. Kama umeamua kujitoa, acha tabia zinazokurudisha ndani ya uhusiano. Punguza mawasiliano yasiyo ya lazima, ufuatiliaji wa mitandao na kutafuta uthibitisho kila mara. Mipaka si chuki; ni namna ya kulinda afya yako ya kihisia. 5️⃣ KUBALI MAUMIVU YA KUACHILIA Usitarajie moyo wako kupona mara moja. Unaweza kumkumbuka na bado usirudi. Unaweza kumlilia na bado ukachagua kuondoka. Kumkosa mtu si ushahidi kwamba unapaswa kurudi kwake. 6️⃣ RUDISHA MAISHA YAKO KWAKO Anza tena kujenga maisha yako bila kuyafanya yaegemee uwepo wa mtu huyo. Rudi kwenye malengo yako, kazi, familia, marafiki, afya na maendeleo binafsi. Usingoje mtu abadilikе ndipo wewe uanze kuishi. Chagua amani yako bila kujiona mwenye hatia. 🧠 JAMBO LA KUZINGATIA ZAIDI. Huwezi kulazimisha mtu akupe aina ya upendo, commitment au usalama wa kihisia ambao hayuko tayari kutoa. Wakati mwingine kujiondoa si kushindwa katika mapenzi; ni kutambua kwamba kuendelea kubaki kunakugharimu zaidi kuliko kuondoka. ❤️ UJUMBE WANGU KWAKO. Kama umejiona katika somo hili na unapitia changamoto ya mahusiano, hisia au uamuzi unaokuchanganya, usibebe kila kitu peke yako. Unaweza kuwasiliana nami kwa ushauri na mwongozo zaidi. 📲 0787515960 Psycho–William Paul Psychology • Relationships • Emotional Well-being

About