@dr.kalobo: mtindo wa maisha una mchango mkubwa sana kwenye acid reflux. 1. Ratiba mbaya ya kula Kuchelewa kula, kula usiku sana, au kulala mara tu baada ya kula huruhusu tindikali kurudi juu kirahisi. 2. Kula kupita kiasi Tumbo likijaa sana, shinikizo huongezeka na acid hupanda juu kwenye umio. 3. Vyakula fulani mara kwa mara Mafuta mengi, pilipili, kahawa, soda, vyakula vya kukaanga na vya tindikali vinaweza kuchochea reflux. 4. Uzito kupita kiasi Mafuta ya tumboni huongeza presha kwenye tumbo na kusukuma acid juu. 5. Mavazi yanayobana tumbo Nguo zinazobana sana huongeza shinikizo tumboni. 6. Msongo wa mawazo (stress) Stress haileti acid moja kwa moja, lakini huongeza dalili na kuharibu mmeng’enyo. 7. Kuvuta sigara au pombe Hulegeza valve ya umio (LES), hivyo acid hurudi juu kwa urahisi.#southafrica #congo #saudiarabia #tonsels #acid
kalobo health care
Region: TZ
Monday 02 February 2026 10:29:11 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @dr.kalobo, please go to the Tikwm
homepage.