@dijahnaafya2: Mmeng’enyo wa chakula ni mchakato ambao mwili hutumia kuvunja chakula tunachokula ili kibadilike kuwa virutubisho vinavyoweza kufyonzwa na kutumiwa na mwili kwa nguvu, ukuaji na afya. Mmeng’enyo wa chakula huanzia wapi? • Mdomoni – chakula hutafunwa na kuchanganywa na mate • Tumboni – asidi na enzymes huvunja chakula zaidi • Utumbo mdogo – virutubisho hufyonzwa • Utumbo mkubwa – maji hufyonzwa, uchafu hutengenezwa kuwa choo