@mr.jibeni.classic: #vdeoviraltiktok🤣🤣🤣🤣 #AFRICAN #comedy #videotiktok #Videotrend follow me my fans📺📺

Mr Jibeni Classic
Mr Jibeni Classic
Open In TikTok:
Region: ZM
Thursday 12 February 2026 08:02:30 GMT
543
10
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @mr.jibeni.classic, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Jeshi la Magereza limefafanua utaratibu wa upunguzaji wa vifungo kwa wafungwa, likisisitiza kuwa hauhusiani na kuhesabu “usiku na mchana” kama baadhi ya wananchi wanavyodhani, bali unazingatia sheria na kanuni zilizowekwa. Kamishna wa Huduma za Urekebu wa Jeshi la Magereza, CP Amina Kavirondo, ameyasema hayo wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea miradi ya Magereza katika maeneo ya Msalato na Vyeyula jijini Dodoma. Amesema mara nyingi kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoshangaa kuona wafungwa waliokuwa wamehukumiwa vifungo virefu wakitoka mapema, huku wakihusisha hali hiyo na vitendo visivyo halali. “Wapo wanaosema tumekuwa tukihesabu usiku na mchana ndiyo maana wafungwa wanatoka mapema. Hii si kweli. Tunafuata sheria. Mfungwa ana haki ya kupata punguzo la theluthi moja (1/3) ya kifungo chake mara tu anapoingia gerezani, isipokuwa kwa wafungwa wa maisha au wale wa adhabu ya kunyongwa,” amesema CP Kavirondo. Amefafanua kuwa kwa mfano, mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30, kisheria anaweza kutumikia miaka 20 kutokana na punguzo hilo, endapo atazingatia nidhamu na taratibu za gereza. Kutokana na hilo, amewataka wananchi kuacha kudhani kuwa askari wa magereza wanahusika na vitendo vya rushwa pale wanapoona wafungwa wakitoka mapema, akisisitiza kuwa taratibu zote zinafanyika kwa mujibu wa sheria. “Wasidhani askari wamekula fedha. Hii ipo kisheria na imewekwa makusudi ili kumpa mfungwa matumaini na kumjenga kisaikolojia aweze kuishi gerezani kwa utulivu na kufuata maelekezo,” ameongeza. Aidha, amesema mbali na punguzo hilo la kisheria, pia kuna misamaha mbalimbali ikiwemo ile ya Rais, pamoja na mifumo ya vifungo mbadala kama parole, ambapo mfungwa anaweza kutumikia sehemu ya kifungo chake gerezani na kumalizia nje chini ya uangalizi. CP Kavirondo amesisitiza umuhimu wa jamii kubadili mtazamo hasi dhidi ya wafungwa, akieleza kuwa si sahihi kuamini kuwa kila anayehukumiwa lazima amalize kifungo chake chote gerezani. “Wananchi waondoe ile dhana ya adhabu pekee (punitive perception). Lengo si kumkomesha mtu kwa kumweka gerezani muda wote, bali ni kumrekebisha ili arejee katika jamii akiwa bora,” amesema. #UhondoTVUPDATES

About