@doctornoel: Kila mtu aliyesoma boarding amewahi kusikia hii story 😅 Kwamba wapishi wanaweka mafuta ya taa kwenye chakula ili kupunguzia wanafunzi hamu ya kufanya mapenzi. Lakini ukweli ni huu 👇 ❌ Mafuta ya taa si dawa ya kupunguza hamu ❌ Hayana uwezo wa kubadilisha homoni za mwili ❌ Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha hilo ❌ Kuweka mafuta ya taa kwenye chakula ni hatari kiafya (Poisonous) Mafuta ya taa ni poisonous, huharibu mapafu (hasa yakivutwa), kuleta kichefuchefu, kutapika na madhara mengine makubwa. Sasa kwanini wanafunzi huhisi kama hamu inapungua wakiwa boarding? ✔️ Mazingira mapya ✔️ Ratiba kali ya shule ✔️ Uchovu ✔️ Stress ya masomo ✔️ Kukosekana kwa faragha Haya mambo yanaathiri psychology na hisia na sio mafuta ya taa.