@healthywithflorence: *Vinyama Vya Ajabu Sehemu Za Siri, Usivichukulie Poa —Inaweza Kuwa Genital Warts (HPV)..!* Kuna mtu alinieleza kisa chake… > “Asubuhi moja nilipoamka, niliona kama vinyama vidogo sehemu zangu za siri, Sikuona maumivu, sikuona usaha, wala sikuona hatari yoyote, Nikadhani labda ni kawaida tu ya ngozi Nikavipuuzia..” Lakini kumbe alichokiona hakikuwa cha kawaida ilikuwa ni Genital warts.... Vinyama vya ajabu vinavyoanza kidogo, bila dalili za maumivu au kuwasha, kisha huendelea kukua kimya kimya..... *Ipo hivi...* Genital warts husababishwa na kirusi kinachoitwa HPV – Human Papillomavirus.... . Na HPV sio kirusi cha kawaida Kina aina zaidi ya 100+, Na baadhi yake husababisha saratani ya shingo ya kizazi, uume, njia ya haja kubwa na hata koo..... . Tatizo kubwa ni kwamba mtu anaweza kuwa na HPV bila dalili zozote...☠️ . Hata kabla hujaona chochote, tayari unaweza kuwa unaambukiza wengine, Ndiyo maana inaitwa bomu la kimya kimya mwilini... *Sasa, vinyama hivi unavyoviona vinaweza..* — Kukua na kuenea zaidi ndani ya mwili... — Kushusha hamu ya tendo la ndoa na kukuathiri kisaikolojia... — Na kwa muda mrefu, vikachangia saratani na matatizo ya uzazi.... *Lakini kuna njia za kujilinda...* — Tumia kondomu (ingawa sio kinga ya 100%). — Kuwa na mwenzi mmoja wa kudumu. — Pata chanjo ya HPV mapema. — Pima afya mara kwa mara hata bila dalili. Na ukishaviona vinyama hivi usiogope, Tiba ipo Lakini kumbuka, tiba huondoa vinyama, si kirusi chenyewe, Ngome yako kubwa ni kinga ya mwili.. Hii ndio sababu hutakiwi kubeza dalili zozote za ajabu kwenye mwili wako.... Kwa sababu afya yako na ya mpenzi wako ni thamani isiyo na kipimo... MB: Genital warts siyo vinyama vya kawaida –Ni alama kwamba HPV bado ipo ndani ya mwili wako. Na kama hautatibu mapema, na hutaimarisha kinga ya mwili wako, vina tabia ya kujirudia tena na tena kama kivuli kisichoisha. ↳ Usiache HPV ikutafune... ↳ Usikae kimya ukiwa na dalili... ↳ Usipuuze kinga yako ya mwili, Ndiyo silaha yako kubwa zaidi... *Kama daktari ningekuambia jambo moja tu leo, ni hili...* 👇 Kuchelewa kuchukua hatua ni sawa na kutoa ruhusa HPV ikuandikie mustakabali wa afya yako. Chukua hatua sasa tambua, pima, tiba, na linda mwili wak, Afya yako na ya mpenzi wako ni uwekezaji mkubwa kuliko chochote...🩺 #lisheboraafyabora #AfyaYaKiume #wanawake #tiktok #nguvuzakiume
Healthy with florence
Region: TZ
Sunday 22 February 2026 18:17:11 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @healthywithflorence, please go to the Tikwm
homepage.