@dkt_mahera: Leo nimeendelea kuimarisha sekta ya elimu katika Jimbo la Butiama kupitia zoezi la ugawaji wa vitabu kwa wanafunzi wetu. Nimepata nafasi ya kutembelea Shule ya Sekondari Butuguri pamoja na Shule ya Sekondari Busegwe (Nimrod Mkono) ambapo tumekabidhi vitabu vya masomo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu wa wanafunzi wetu. Hatua hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata rasilimali muhimu za kujifunzia, ili kuwajengea msingi imara wa elimu na kuwaandaa vyema kwa maisha yao ya baadaye. Tunaamini kuwa uwekezaji katika elimu ni uwekezaji wa moja kwa moja katika maendeleo ya Butiama na taifa kwa ujumla. Tutaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wanafunzi wetu wanapata fursa bora za kujifunza. #ElimuKwanza #ButiamaInaendelea #KaziInaendelea