@neno_kuntu: NIMECHOKA SANA 😭😭😭 Machozi haya si dalili ya huzuni tu pekee, bali ni maelezo niliyoshidwa kuyaeleza hata kwa lugha ya maandishi Moyo wangu umejaa mambo mengi mazito, ambayo sina uwezo wa kuyahimili tena rohoni mwangu Nina macho ila sioni tena ninapokwenda, nina akili ila siwezi tena kufikiria Joto la hisia linafuka moshi mwilini mwangu, kila nikijiinamia chini natamani nisinyanyuke tena Nimepambana kwa maombi ila bado sioni njia, nimekubali kuwa na subira ila maumivu yananielemea Kila siku nazidi kujipuuza, nimeishiwa nguvu hata ya kuituliza nafsi yangu, wale walionifanya kioo sioni kama ninahaki ya wao kuniangalia Najihisi bahati nzuri zipo kwa ajili ya wenzangu tu, bahati mbaya ndilo fungu lipo kwa ajili yangu Kwa nini njia yangu ngumu kiasi hiki? ninakosea wapi? Ni nani anayegawa riziki akifika kwangu haoni jitihada zangu? Sina shida na vingi bali nipate walau kidogo cha kustiri aibu zangu, sina shida na kesho bali walau niimudu vizuri leo yangu Naogopa kusema mbele ya hao wanaonitegemea ila nafsi yangu inajua kuwa NIMECHOKA SANA 😭😭 Eee Mola wangu kama unasikia kilio hiki ni mimi tena mja wako dhalili nimekuja tena mbele zako Nadhalilika kwa watu ila tambua tumaini langu bado lipo kwako Nanyanyasika kwa watu ila najua starehe ipo kwenye miliki yako Naumizwa na watu ila bado naamini mwenye upendo wa kweli atakuja kwa idhini yako Nasemwa na watu ila ukweli wa moyo na roho yangu unaujua wewe peke yako Naomba nipe bila kuangalia makosa yangu, maana sina wa kumtegemea zaidi yako 🙏🙏 #ujumbemzuri📩 #huzuni #tanzaniatiktok #kenyantiktok🇰🇪 #nenokuntu

@neno_kuntu
@neno_kuntu
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 03 March 2026 16:10:25 GMT
1828
42
1
9

Music

Download

Comments

yuma.fidel.awazi
Yuma fidel Awazi :
😁
2026-03-11 11:17:59
0
To see more videos from user @neno_kuntu, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About