@husseinmiladu: ASSALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKAATUH Kwa heshima na taadhima, tunakualika katika hafla adhimu ya AHLU ZAMAAN – Siku ya Watu wa Zamani na Mapenzi ya Bwana Mtume Muhammad ﷺ. Huu ni Msimu wa Pili wa Ahlu Zamaan, tukihuwisha turathi za wazee wetu kwa tungo za qasida zenye mawaidha na mapenzi ya Mtume ﷺ, tukijenga imani, nidhamu na mshikamano. 📍 Mahali: Ukumbi wa DYCC, mkabala na Yemen School 📅 Tarehe: 28/03/2026 🕐 Muda: Saa 1:00 usiku hadi saa 5:30 usiku. Karibuni nyote tushiriki pamoja katika mapenzi ya Mtume ﷺ. AHLU ZAMAAN – UPENDO, NIDHAMU NA MSHIKAMANO.