@pata.habari: “Hata wewe shoga yangu?” 🎶🔥 Hii ni mistari iliyowahi kuteka masikio ya wengi kutoka kwa mwanadada wa Kizaramo SHAA, aliyekuwa chini ya usimamizi wa gwiji wa muziki Master Jay. Kwa kipindi hicho, sauti yake laini lakini yenye hisia kali iliweza kutikisa anga la muziki wa Bongo Fleva na kuwafanya mashabiki wengi kuimba kila mstari kwa hisia. 🎤✨ Ni moja ya nyimbo zilizobeba ujumbe mzito wa mapenzi, maumivu na usaliti, huku melody yake ikibaki kichwani mwa watu hadi leo. 💔🎶 Hakika, Shaa aliweka alama yake kwenye historia ya muziki wa Tanzania! 🇹🇿🔥 Unakumbuka ulipoisikia kwa mara ya kwanza? #fyp #tiktoktanzania #tiktokviral