@dr.kishimba: ✅Madhara Makubwa ya Kisukari Kwa Mtu Asiyekidhibiti Kisukari kisipodhibitiwa mapema, huanzia kwenye dalili ndogo hadi madhara makubwa ya mwili. Haya ndiyo madhara makubwa ambayo kila mtu anatakiwa ajue: ✅Macho – Upofu Kisukari huathiri mishipa ya damu ya macho na kusababisha: Kuona ukungu Macho kudhoofika Upofu kabisa kama hakitadhibitiwa ✅Figo – Kushindwa Kufanya Kazi Sukari ikikaa juu muda mrefu huichosha figo na kusababisha: Kuvuja kwa protini kwenye mkojo Figo kushindwa kufanya kazi kabisa ✅Vidonda Sugu & Kukatwa Viungo Kisukari hupunguza mzunguko wa damu na kuharibu neva, hivyo: Vidonda haviwezi kupona Vidonda kukolea hadi kukatwa mguu ✅Kupungua kwa Nguvu za Kiume Kwa wanaume, kisukari huathiri mishipa ya damu na homoni: Nguvu za kiume kushuka Hamu kupungua Kusimama kwa shida ✅Kiharusi (Stroke) & Mshtuko wa Moyo Sukari juu huongeza: Shinikizo la damu Mafuta mabaya Kuziba kwa mishipa Hivyo hatari ya stroke na heart attack huwa juu sana. ✅Ganzi, Kuwashwa & Maumivu ya Miguu/Mikono Kisukari huunguza mishipa ya fahamu (neuropathy), hivyo mtu hupata: Maumivu ya moto Ganzi Kuchoma-choma kama sindano ✅Kupoteza Uzito na Uchovu Mkubwa Mwili hauingizi sukari kwenye seli, hivyo mtu: Anachoka haraka Anakonda hata kama anakula ✅Maambukizi Kuongezeka Kisukari hupunguza kinga ya mwili: Fangasi hujirudia Vidonda havitaki kupona Maambukizi ya njia ya mkojo kuwa mara kwa mara #viralvideo #africantiktok #tibalishe #fyp#afyabora.
Dr.kishimba
Region: TZ
Sunday 22 March 2026 09:39:57 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @dr.kishimba, please go to the Tikwm
homepage.