@paza_sauti_media: Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia askari mgambo watatu kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Rashid Masunga Nyandonga (31), fundi simu na mkazi wa Bugando Jeshini, Wilaya ya Nyamagana. Watuhumiwa hao ni Zongoli Richard Makongoro (38), mgambo wa Kata ya Mahina; Genge Chacha Mwita (45), mgambo wa Kata ya Igogo; na Ibrahim Chacha Mwita (25), mgambo wa Kata ya Pamba, wote wakazi wa Wilaya ya Nyamagana. Akizungumza na Waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo lilitokea Machi 20, 2026 majira ya saa 12:45 jioni katika Mtaa wa Mission, eneo la Sahara, Kata ya Pamba, ambapo inadaiwa kuwa askari hao walimtilia shaka marehemu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya mirungi na kumkimbiza kabla ya kumkamata akiwa na kiasi hicho cha dawa. Hata hivyo, wakati wa tukio marehemu alionekana kuishiwa nguvu na baadaye alipelekwa Hospitali ya Sekou Toure kwa matibabu, ambapo alifariki dunia akiwa anapatiwa huduma. Aidha, askari hao walifanya ukamataji huo bila kuwapo kwa operesheni rasmi ya jeshi hilo, na tayari wamekamatwa kwa mahojiano huku uchunguzi ukiendelea. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi, huku polisi wakiendelea na uchunguzi ili sheria ifuate mkondo wake.
Paza Sauti
Region: TZ
Sunday 22 March 2026 16:06:13 GMT
Music
Download
Comments
jumaaMartin14 :
Pole sama bimkubwa innalilah wa innailayh raju-uun🤲
2026-08-07 14:42:12
0
ARISTIDIA :
Pole sana mama mu gu akupe moyo wa uvumilivu tena na tena
2026-08-11 18:48:28
0
Johnjoseph :
pole sana kwa familia, Viongozi wa Mwanza wanasubili mwananchi afe ndio wajitokeze hii nchi kunahaja ya kutafakari sana.kunamatukio Mengi sana.
2026-03-22 17:41:28
2
ANCLE :
pole san
2026-05-23 20:17:39
0
fatmamalesa :
pole sn mama kwa maumivu unayo yaisi moyoni poleeeee sanaaaa
2026-03-24 10:19:37
1
Aminahnasry🌹🌹 :
🥰
2026-08-02 10:17:48
0
To see more videos from user @paza_sauti_media, please go to the Tikwm
homepage.