@tsharifu_dume_de_yamal44: Rakaa ni nini? Cha kwanza ni muhimu ufahamu maana ya Rakaa, Rakaa ni kipindi kimoja cha swala hupatikana mtu anapoinuka kutoka baina ya sijda mbili na kusimama wima. Rakaa ni pale umeanza swala yako ukaenda rukuu, ukainuka na ukaenda sujud kisha ukakaa kitako na ukasujudu tena ukiinuka hiyo ni tayari rakaa moja. Kila swala ina rakaa zake Mfano Salatul Fajr ina rakaa mbili. Salatul Dhuhr ina rakaa Nne Salatul Asr ina rakaa Nne Salatul Magharibi ina rakaa tatu Salatul Ishaai ina rakaa Nne. Kila utakapo inuka toka katika sijda mbili na kusimama wima basi utahesabu kama rakaa ingine. Kwa swala zenye Rakaa Nne na Tatu, basi kuna Tahiyyat mbili, 1) Tahiyyat ndogo na 2) Tahiyyat kubwa (ambayo ni ya mwisho). Katika swala za Asr, ishaai na Dhuhr kuna attahiyat kila baada ya rakaa mbili (Tahiyyat ndogo na ya pili ni kubwa na kutoa Salamu) Salatul Magharibi ina rakaa tatu hivyo katika rakaa ya pili utakaa Tahiyyat na rakaa ya tatu utakaa Tahiyyat kubwa ambayo ni ya mwisho. Salatul Fajr ina rakaa mbili hivyo ukikaa Tahiyyat moja katika rakaa ya pili basi ndio Tahiyyat kubwa na ya mwisho.. @nakupenda_allah

𝐌𝐀𝐍'𝐃𝐇𝐀𝐋 𝐒𝐇𝐀𝐑𝐈𝐅𝐔
𝐌𝐀𝐍'𝐃𝐇𝐀𝐋 𝐒𝐇𝐀𝐑𝐈𝐅𝐔
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 27 March 2026 06:08:50 GMT
582
73
0
2

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @tsharifu_dume_de_yamal44, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About