@lihekamedia: Tujikumbushe kidogo Safari ya Tanzania one @hassanmwakinyojr ilipoanza kushika hatamu katika ulimwengu wa boxing kimataifa zaidi Ilikuwa september 8, 2018 pale katika ardhi ya Uingereza ambapo Mdigo kutoka Tanga Aliijenga heshima ya Taifa la tanzania katika mchezo wa Boxing mara baada ya Kumtembezea Mkong'oto mkali Mpinzani wake Sam Engginton na kufanikiwa kumpiga kwa Technical Knock-out ( TKO ) mnamo raundi ya pili tu ya pambano Pambano hilo lilifanyika katika mji wa Birmingham kwenye ukumbi wa Birmngham Arena, usiku huo Champez Hassan mwakinyo alipewa jina la "Super punch" kutokana na uzito wa makonde yaliyokuwa yakimiminika kama mvua usoni kwa Sam Enggington, Ndani ya muda mchache tu ilikuwa ni kama anapigana Korogwe kutokana na wafuasi alio wapata baada ya kuonyesha mchezo mzuri Kwenye Boxing Tanzania Mwakinyo ndiye Baba wa Imani. @hassanmwakinyojr