@chawamata_tv: VIDEO: Mbunge wa Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani, ameishauri serikali kuangalia upya kiwango cha posho kinacholipwa kwa madiwani pamoja na wenyeviti wa vijiji ili kuendana na majukumu makubwa wanayotekeleza katika ngazi za msingi za uongozi. Akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katika Bunge la Tanzania linaloendelea jijini Dodoma, Katani alisema viongozi hao wamekuwa wakifanya kazi kubwa katika kusimamia maendeleo ya wananchi lakini motisha wanayoipata bado ni ndogo. Mbunge huyo ameeleza kuwa madiwani na wenyeviti wa vijiji ndiyo viongozi wa karibu zaidi na wananchi, hivyo wanakutana na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, ikiwemo kushughulikia migogoro ya kijamii, kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi. Aidha, amegusia pia suala la usafiri kwa viongozi hao wa ngazi za vijiji akisema wengi wao wanakabiliwa na changamoto ya kufika kwa haraka katika maeneo yenye matatizo kutokana na ukosefu wa usafiri. Amependekeza serikali iweke utaratibu wa kuwapatia pikipiki viongozi hao ili kuwasaidia kufika kwa urahisi katika maeneo yenye changamoto na hivyo kuongeza ufanisi katika utatuzi wa matatizo ya wananchi. Katani amesisitiza kuwa mchango wa madiwani na wenyeviti wa vijiji katika maendeleo ya jamii ni mkubwa, hivyo ni muhimu serikali kuimarisha mazingira yao ya kazi kwa kuwapatia motisha stahiki ikiwa ni pamoja na kuongeza posho na kuboresha usafiri wao. #chawamata_tv
CHAWAMATA TV
Region: TZ
Saturday 11 April 2026 13:26:44 GMT
Music
Download
Comments
vailethwilliam :
Hongera sana Mheshimiwa kwa kuliona hili 🥰
2026-04-18 07:57:21
0
Subuya@ D :
hongera sana mzee
2026-04-13 02:58:18
0
mohamedkitogo8 :
Hongera sana mbunge wulewa kuwasemea madiwani iyo mingine imekaa tu kimya
2026-04-11 19:36:00
1
Assanal Kumtipa :
🙏🙏hakika tupewemadiwani tunateseka
2026-04-13 21:19:50
0
Zainabu Mohamedi :
@na wadau wamaendeleo ya kata je maana tunachangia michango mikubwa
2026-04-15 20:32:42
0
kufakulala :
mwenyekiti wa mtaa Hana posho yoyote je hiyo ni sawa
2026-04-12 18:46:59
0
Devi :
ubalikiwe
2026-04-11 19:50:46
0
selesti :
vp watu wakawaida
2026-04-11 17:45:46
0
kalimu manya :
Sina la kusema kabisa kwako ongela
2026-04-16 12:56:52
0
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm
homepage.