@kanikibrown: Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameagiza kufutwa kwa leseni 40 za utafutaji madini baada ya wamiliki wake kushindwa kutekeleza masharti licha ya kupewa hati za makosa na muda wa kurekebisha dosari zilizobainika. Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mhe. Mavunde ameielekeza Tume ya Madini kufuta leseni hizo mara moja na kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, huku akisisitiza kuchukuliwa hatua kali dhidi ya leseni zote zitakazobainika kutotekelezwa ipasavyo. Aidha, amebainisha kuwa tarehe 10 Aprili 2021, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini ilitoa hati za makosa kwa leseni nyingine 43, zikiwemo leseni 40 za utafutaji madini na leseni tatu za uchimbaji (mining licenses). Wamiliki wa leseni hizo walipewa siku 30 kurekebisha kasoro, na watakaoshindwa leseni zao zitafutwa ili kutoa nafasi kwa wawekezaji wengine, wakiwemo wachimbaji wadogo. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu matukio ya “gold rush” yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, huku ikichukua hatua madhubuti kulinda usalama wa wananchi, mali zao na kuhakikisha uzingatiaji wa sheria na kanuni za madini. Amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, shughuli zote za uchimbaji madini lazima zifanyike kwa kuzingatia umiliki halali wa leseni. “Ni muhimu kueleweka kuwa uchimbaji wowote wa madini bila leseni halali ni kinyume cha sheria, na Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya wanaokiuka taratibu hizi,” alisema Mavunde. Ameongeza kuwa hatua hizo pia zinalenga kuzuia migogoro kati ya wachimbaji na wamiliki halali wa leseni, kulinda mazingira dhidi ya uharibifu unaotokana na uchimbaji holela, pamoja na kudhibiti hatari za milipuko ya magonjwa katika maeneo ya migodi. #WEWENIFAMILIA Ripota wa Habari za Mikoani ✍ @kaniki_brown “Endelea kufuatilia #Ripotawahabarizamikoani kwa taarifa sahihi na za uhakika. KWA MATANGAZO YA BIASHARA NA HABARI Follow kwa updates zaidi. Kuwasiliana 📞 0622732287 #kanikibrown”
Kaniki Brown
Region: TZ
Wednesday 15 April 2026 07:55:25 GMT
Music
Download
Comments
user6195266151744 :
safi kaka
2026-04-15 18:54:16
1
Yusuph Muna :
hapo Sawa
2026-04-16 15:07:12
1
Amos :
naomba mimi moja 1
2026-04-15 19:30:56
0
tdmunyamwezi12 :
mia
2026-04-16 12:52:18
0
Yohana bright :
naya msasa ifute
2026-04-17 19:45:49
0
Raulian Kipeah :
msasa je haifuti
2026-04-18 12:09:10
0
Alhamdulillah :
Nipeni mimi
2026-04-19 11:09:45
0
To see more videos from user @kanikibrown, please go to the Tikwm
homepage.