@afyabora26: 🏃♂️ MAZOEZI NA MMENG’ENYO WA CHAKULA Mazoezi ni njia rahisi lakini yenye nguvu ya kuimarisha mmeng’enyo wa chakula. Huhitaji kufanya mazoezi makubwa—hata yale ya kawaida unayoweza kufanya chumbani au nje yanatosha. Kwa nini mazoezi ni muhimu kwa mmeng’enyo? 1️⃣ Huchochea utumbo kufanya kazi Mazoezi husaidia kusukuma chakula kwenye utumbo, hivyo kupunguza 👉 kufunga choo na gesi 2️⃣ Hupunguza asidi tumboni Husaidia kudhibiti 👉 Acid Reflux na kiungulia 3️⃣ Huboresha mzunguko wa damu 👉 Mwili hupata virutubisho vizuri 👉 mmeng’enyo huwa imara 4️⃣ Hupunguza msongo wa mawazo Stress huathiri sana tumbo 👉 mazoezi husaidia kuutuliza mwili na akili ⏰ Ufanye lini mazoezi? ✔ Asubuhi baada ya kuamka ✔ Au jioni/usiku baada ya kula (subiri angalau dakika 30–60) Mazoezi gani yafanyike? Huhitaji gym—anza na haya: 1. Kutembea dakika 15–30 hasa baada ya kula 👉 husaidia mmeng’enyo kuanza kazi 2. Kupanda ngazi dakika chache tu 👉 huchochea mwili na utumbo 3. Stretching (kunyoosha mwili) asubuhi au jioni 👉 huamsha mfumo wa mmeng’enyo 4. Mazoezi mepesi ya tumbo kama kukaza na kuachia tumbo 👉 husaidia utumbo kufanya kazi vizuri Epuka kufanya mazoezi makali mara tu baada ya kula kulala bila hata kutembea kidogo baada ya kula 👉 Mazoezi madogo kila siku = mmeng’enyo mzuri 👉 Sio lazima gym—anza na unachoweza Unapata changamoto za mmeng’enyo kama gesi, kiungulia au choo kigumu? 👉 Anza mazoezi leo + pata mwongozo sahihi 📲 0768 342 937 @AFYA BORA