@ekmunyagi: Kila anayemiliki hisa ya kampuni anastahili kupata gawio. Hata hivyo, ili ulipwe gawio, ni lazima uwe mmiliki wa hisa hizo tarehe ya mwisho ya kipindi cha CUM DIV. Kwa mfano, kwa CRDB Bank Plc, tarehe ya mwisho ya CUM DIV ni 4 Mei 2026. Hii ina maana kuwa yeyote atakayekuwa anamiliki hisa hizo ifikapo saa kumi jioni (muda wa soko kufungwa), tarehe 4 Mei, atastahili kupokea gawio litakalolipwa tarehe 1 Juni 2026. Lakini kama utanunua hisa kuanzia tarehe 5 Mei 2026, hutapata gawio hilo — itabidi usubiri hadi gawio la mwaka unaofuata, endapo bado utakuwa unamiliki hisa hizo. #Uwekezaji #Hisa #Gawio #DSE #ElimuYaFedha
Edmund Munyagi
Region: TZ
Tuesday 21 April 2026 18:24:06 GMT
Music
Download
Comments
Millan :
Mwaka gani huo
2026-05-17 18:44:33
0
Nah 🍁 :
Nauliza mimi niliyejiunga na kununua hisa mwezi huu wa nne je nitaweza pata gawio au had gawio la mwakani??
2026-04-21 19:41:19
0
Dr julius🔬 :
je kupata gawio n unajaza fomu
2026-04-22 12:58:40
0
B I G C H A W A :
Je mfano ukawa una nunua tuu hisaa ila gawio unend kuchukua mybe miaka 5 je zinakuwepo zote za miaka 5 au ndo gawio la mwaka huo huo
2026-04-21 18:29:57
0
R.A.weston :
samahani, kuna hisa nilinunua mwezi wa pili lakini hadi leo ziko suspended, sasa hata broker hawajawah pokea simu , pia kuna baadhi niliuza mwezi wa pili lakini bado hadi leo hakuna matokeo, nifanye nini??
"nahisi kupoteza pesa"
2026-04-26 15:13:23
0
To see more videos from user @ekmunyagi, please go to the Tikwm
homepage.