@radiographer_noah: Kumsikia mtoto akicheza tumboni – hatua kwa hatua 🔹 Wiki 0–16 [miezi 4] (ikiwa ni mimba ya kwanza) Ni kawaida kabisa HAUMSIKII mtoto akicheza tumboni. 🔹 Wiki 17–20 [miezi 5] Mama wa mimba ya kwanza huanza kumsikia taratibu (kama vitu vidogo vidogo). Kwa waliowahi kuzaa, wanaweza kusikia mapema kidogo. 🔹 Wiki 20–24 [miezi 6] Mtoto huanza kusikika vizuri zaidi, lakini bado si kila wakati. 🔹 Wiki 24–28 [miezi 7] Mtoto anacheza lakini si kwa mpangilio maalum. Kuna vipindi vya ukimya (analala/anapumzika), lakini mama anapaswa kumsikia mara kadhaa kwa siku. 🔹 Baada ya wiki 28 Mtoto anapaswa kumsikika kila siku kwa mpangilio fulani. 👉 Akipunguza Kucheza au Ukawa Haumsikii kwa muda mrefu (kama masaa 10–12) → nenda hospitali(Utapima Ultrasound Kuhakikisha Mtoto Yupo Sawa) au Wasiliana na daktari siku hiyo hiyo. ‼️⚠️KUMBUKA⚠️‼️ Maelezo haya ni kwa ajili ya elimu tu na kuongeza uelewa. Si maelekezo ya kitabibu. Ni muhimu kufuata ushauri wa daktari wako au kliniki. #mtoto #kucheza #ultrasound #trendingvideo #aitiktok