@mtumbaplus: Baada ya Kifo Cha Mume Wangu Niliifungua Simu Yake… Nilichokiona Kimenifanya Kuchanganyikiwa! · Miaka 5 alikua ni Mtu wa pombe na kulala nnje nikajua ni wanawake! Nilikuta meseji moja tu kutoka kwa mume wangu, iliandikwa, “Mke wangu nimechoka, nimechoka sana.” Hakuandika kitu kingine chochote na mimi badala ya kumjibu vizuri, nilimjibu, “Ndiyo lazima uchoke na umalaya wako, si hutaki hata kukaa nyumbani, kila siku ni pombe tu na malaya wako, choka mpaka u*f*ilie mbali.” Nilimtumia ile meseji kisha nikaanza kumpigia mfululizo, hakupokea, hakujibu, hakufanya chochote. Aliendelea kukaa kimya, nilituma meseji nyingine zaidi ya (50) nikitaka kujua yuko wapi lakini hakujibu hata moja. Baada ya hapo simu yake nikipiga ilikuwa haipatikani. Niliishia kutu*kana na nikapanda zangu kitandani nikalala. Nilifanya hivyo nikijua ni tabia ya mume wangu. Kwa miaka kama (5) hivi ya mwisho ya ndoa yetu alikuwa amebadilika, haongei na mimi kama zamani, alikuwa ni mtu wa pombe na mara nyingi mkigombana kidogo anakaa kimya hataki hata kuongea anaondoka anarudi labda baada ya siku mbili. Nilishamshirikisha mama yake, wakwe, ndugu zake, kwa mchungaji na kila sehemu lakini kamwe hakuwahi kuenda na alikuwa akiitwa anaomba msamaha hasemi shida ni nini, anasema nisamehe mke wangu nitajirekebisha lakini hajairekebishi. Mara nyingi alikuwa akitaka kuongea na mimi basi nitamlalamikia, nakumbushia mambo ya nyuma mpaka ananiambia shida yako husikilizi, basi anakaa kimya. Siku hiyo nililala kama kawaidaa! Kesho yake asubuhi alikuwa bado hajarudi, niliwaandaa watoto kwa ajili ya shule lakini siku hiyo wote ni kama waligoma kwenda shule, walikuwa wanalia tu hawana raha. Nikashia kufoka ukichanganya na hasira za baba yao nililazimika hata kuwa*pi*ga, nik*ac*hapa nikafanya kila kitu lakini waligoma kabisa kwenda shule. Mwisho nikawaambia mtajua wenyewe. Nikatoka zangu kwenda kazini nikiwa na hasira sana. Nilifika kazini nikiwa nimechelewa ila saa (3) asubuhi nikapigiwa simu, alikuwa ni mama mkwe wangu akaniuliza uko wapi. Nikamuambia nipo kazini, akaniambia sawa, nikataka kumuambia kuhusu mume wangu kuwa hajarudi akaniambia usijali, kuna mtu anakuja kukuchukua, mama alionga kwa sauti kama ya huzuni kama najikaza. Nilishituka kidogo kwani kunichukua kivipi, mama mkwe alikuwa ananipenda kwa kuwa tangu mtoto wake kubadilika mimi ndiyo nilikuwa nabeba majukumu mpaka kuwahudumia wao sasa ananichukua akina nani. Ile sijakaa sawa shemeji yangu akaja na bajaji, akaniambia ingia. Nilishangaa boss wangu anairuhusu kirahisi, basi nikaingia. Nikafika kwenye bajaji namuuliza vipi shemeji kwa kama analengwa-lengwa na machozi, namuuliza vipi ndiyo akaniambia “shemu boro hatunaye.” Hicho ndiyo kitu pekee nilisikia nilidondoka na kupoteza fahamu, bila kujijua kama nilikuwa nampenda mume wangu kihivyo. Nikaja kuzinduka niko hospitalini watu wamenizunguka wananiangalia kama mgonjwa wa leo kesho. Nikataka kujua kuhusu mume wangu wakanizuia sana ila nikawaambia hapana, nataka kujua, basi wakaniambia alikutwa amefariki bar. Alikunywa sana akalala kwenye meza kama kawaida yake, yaani wahudumu wakasema ni kawaida yake kunywa mpaka kulala ila baadaye wakamkuta kashafariki. CCTV kamera zinaonyesha hakuna mtu alimgusa wala nini ila alikunywa sana tangu saa kumi jioni mpaka saa tisa usiku na anachanganya pombe huku hajala kitu chochote. Basi nilijitahidi nikatoka pale. Kweli niliu*mia hasa nikikumbuka jinsi ambavyo nilikuwa naongea naye, meseji za mwisho nilizomtumia. Nilirudi nyumbani nikakabidhiwa vitu vyake kama simu, nikachukua simu, hakuna aliyeifungua kwani mimi pekee ndiyo nilikuwa najua password. Niliingia na kufuta meseji zote nilizokuwa nimemtumia. Lakini katika kuangalia meseji nyingine ndiyo nikaja kugundua kuwa kwa miaka mitano mume wangu alikuwa hana kazi. Yaani kipindi anabadilika hata yale ya pombe alikuwa amesimamishwa kazi. Nilikuta email zake akihangaika kuomba kazi sehemu mbalimbali na nyingine akilalamika kwa marafiki zake .PART 02👉👉👉 #moment #life #creatorsearchinsight

MTUMBA PLUS
MTUMBA PLUS
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 30 April 2026 05:18:07 GMT
392031
4884
180
633

Music

Download

Comments

hans.donny
Hans Donny :
wanaume tunapitia mengi sana jamn funzo hilo
2026-05-01 07:12:11
42
emmanuelmwakamele1
Mwakamisa :
samahani, umesema mume wako alikuwa anaitwa "Boro" au nimesoma haraka sana? ni jina lake Boro? Boro kama Boro?
2026-05-01 16:24:27
22
martha_braids
Martha braids :
mtu anitumie voice note Maana ni ndef
2026-04-30 21:15:29
20
warida144
warda makuka :
mh pole.sana kipenz mungu akutie nguvu ya kulea watoto. pole sana.
2026-04-30 18:34:00
7
george.costar
George costar :
Duuuuh kama kweli pole sana mpendwa
2026-04-30 16:55:17
6
nanah4067
it's- jojoh :
kuna kitu nimejifunza jmn
2026-05-03 05:28:40
6
princess.siphaa
💦Bby princess🦋 :
dah nimekuulumia mia nimemuhulumia zaid mumeo apumzik kwa amani
2026-04-30 12:50:02
4
user1481229610511
agness :
pole sana kipenz, apumzike Kwa amina 🙏🕊️
2026-05-02 19:11:45
3
nashpie2
Nashpie :
wataenda sana....Huyu Mungu Huyu Mungu hatching mja wake
2026-05-01 11:30:37
0
its.femida
FEMIDA🎀♋️🦋 :
Daaaah nashindwa hata kushauri ila Mungu akulinde ww pamoja na watoto wako.ANEN🙏
2026-05-01 18:35:40
3
maria.katembo1
Maria Katembo :
nzuri sana
2026-04-30 19:53:45
0
dinalmmadege
dinalmmadege :
duh aiseeh
2026-04-30 18:20:38
0
upendofelix
upendofelix :
Daah pole sana
2026-04-30 21:19:08
0
suu42882
suu :
dah pole sana inauma sanaa
2026-04-30 16:50:46
0
mariva.mshana
Mariva Mshana :
next
2026-04-30 20:38:03
0
mangulumbas
mangulumbas :
Daa🥹🥹
2026-04-30 14:16:41
0
tauskidoty1
taus USA🇱🇷 :
nmeisoma fb hiii jmn 🥺
2026-05-04 20:22:41
1
neykasian8
ney kasian8 :
Dah🥲
2026-04-30 13:32:32
1
princesstaria1
princesstaria🥰♥️🥰 :
unaniogopesha na mm mme wangu ana io tabia Yani jmn
2026-05-01 05:52:05
1
sakin0299
sakin🍎 :
🥹dahhhh
2026-04-30 15:35:57
4
glorysteph3
Ms.Glory😍 :
Part two please
2026-05-01 16:25:57
1
ncycun
NancyMaro❤️ :
Mbona kama unaniongelea nn jaman🥺
2026-05-19 12:51:05
0
user3030903362995
user3030903362995 :
mwendelezo bas
2026-06-10 12:10:21
0
gladnessmomlaura
Laura moses😘 :
next
2026-06-11 20:01:06
0
bianca.sammy82
Bianca Sammy :
heee mbona nalia
2026-04-30 15:40:39
0
To see more videos from user @mtumbaplus, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About