@tawhidfirst2: Dhikri Za asubuhi أصبحنا وأصبح الملك لله، والحمد لله، لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير. ربِّ أسألك خير ما في هذا اليوم وخير ما بعده، وأعوذ بك من شر ما في هذا اليوم وشر ما بعده، ربِّ أعوذ بك من الكسل وسوء الكِبَر، ربِّ أعوذ بك من عذاب في النار وعذاب في القبر. (Na jioni inasemwa: “أمسينا وأمسى الملك لله” badala ya “أصبحنا…”) 📚 Imepokelewa na Imamu Muslim Tumeingia asubuhi, na ufalme wote ni wa Mwenyezi Mungu. Himdi zote ni zake. Hapana mola wa haki isipokuwa Allah peke yake, hana mshirika. Ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye ana uwezo juu ya kila kitu. Mola wangu! Nakuomba kheri ya siku hii na kheri ya baada yake. Najikinga kwako kutokana na shari ya siku hii na shari ya baada yake. Mola wangu! Najikinga kwako kutokana na uvivu na uzee mbaya. Mola wangu! Najikinga kwako na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburini.” Kauli za Maulama kuhusu dhikri hii 🔹 Imamu An-Nawawi (رحمه الله) amesema: Dhikri hizi ni miongoni mwa adhkār muhimu sana za asubuhi na jioni, na inapasa Muislamu azihifadhi na kuzisoma kila siku. 🔹 Ibn Al-Qayyim (رحمه الله) amesema: Adhkār za asubuhi na jioni ni kama kinga (ngao) kwa Muislamu. Kadiri anavyozidumisha, ndivyo anavyolindwa na shari za dunia na Akhera. 🔹 Ibn Baz (رحمه الله) amesema: Ni Sunnah kusoma adhkār hizi kila asubuhi na jioni, nazo ni sababu ya kupata ulinzi wa Mwenyezi Mungu na kuondolewa madhara.

Aboubakar omba
Aboubakar omba
Open In TikTok:
Region: AE
Monday 04 May 2026 03:00:32 GMT
121
27
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @tawhidfirst2, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About