@iem_pius: 1. Kutegemea ndugu na marafiki ndio wawe wateja wako wakubwa. Watu wanaokupenda sio lazima wanunue bidhaa zako. Wakati mwingine wanakuunga mkono kwa maneno tu. Biashara inayokua kweli hujengwa na watu wasiokujua lakini wanaamini huduma yako. 2. Kuuza kwa mkopo ili uonekane una moyo mzuri. Biashara sio taasisi ya misaada. Ukizoea kutoa bidhaa bila mfumo mzuri wa malipo, mwisho wa siku utaanza kukimbizana na madeni kuliko kutafuta faida. Wengi waliofilisika walikuwa wapole sana kwenye biashara zao. 3. Kushusha bei ovyo ili uuze haraka. Bei ndogo sio kila siku inamaanisha biashara nzuri. Ukikosa kuhesabu gharama zako vizuri utaishia kuuza sana lakini hela haionekani. 4. Kutegemea wateja wa kupita njia pekee. Ukifungua biashara alafu unasubiri tu watu wapite ndipo wanunue… utachoka. Dunia ya sasa inahitaji kujitangaza, kutumia mitandao ya kijamii, kutengeneza mahusiano na kuwafuata wateja. 5. Kuweka faida ya kubahatisha bila kuhesabu gharama zote. Watu wengi wanaongeza elfu moja au mbili juu ya bei ya kununua wakidhani wanapata faida. Lakini hawajapiga hesabu ya kodi, usafiri, umeme, vifungashio, muda na matumizi mengine. Mwisho wa mwezi biashara ipo… lakini maisha hayasogei. 6. Kuzoeana kupita kiasi na watu wa eneo la biashara. Duka au ofisi ikigeuka sehemu ya stori siku nzima, wateja wengine wanaogopa hata kuingia. Biashara inahitaji mazingira yenye utulivu na professionalism, sio kijiwe cha maongezi. 7. Kutunza bidhaa ambazo hazijalipiwa. Naomba uniwekee, narudi kesho…Kesho nyingine haifiki. Bidhaa ikae kwa mtu aliyelipa, sio aliyetoa ahadi. Ukifanya hivi mara nyingi utaanza kufunga mtaji wako mwenyewe. 8. Kutokujifunza kuhusu biashara yako. Biashara sio kufungua duka tu. Lazima ujifunze masoko, huduma kwa wateja, matumizi ya mitandao, na namna ya kutunza fedha. Usipojifunza, ushindani utakutoa sokoni kimya kimya. 9. Kuchanganya hela ya biashara na matumizi binafsi Hili ndio kaburi la biashara nyingi. Leo unatoa hela ya stock kwenda starehe, kesho unakosa mtaji wa kuzungusha.Biashara ikikosa nidhamu ya fedha… kufa kwake ni suala la muda tu. Kama Unataka kuanza biashara kwa mtaji mdogo wa kuanzia sh. 1,000,000/- mpaka 2M Nitumie Ujumbe wenye neno BIASHARA kwenda whatsap number +255756133313 Share ujumbe huu kwa kijana mwenzako ili na yeye ajifunze #tiktok #viral #treanding #trendingreels #trendingvideo
Pius Kichere🇹🇿
Region: TZ
Thursday 07 May 2026 16:50:59 GMT
Music
Download
Comments
Sigisfridy :
umetisha mkuu
2026-06-23 20:15:11
1
Ally Ramadan :
nimeipenda iyo ubalikiwe unacho kisema ni kweli kabisa brother
2026-05-08 16:27:42
9
richardbazil96sim :
yes
2026-05-13 14:57:37
1
Sheby boy TZ :
Nina million 1
2026-05-22 18:10:14
1
annapraise :
hakika bro
2026-05-07 16:55:24
5
riine :
asante
2026-05-23 15:15:20
1
Dickson :
umetixha sana
2026-05-10 17:47:29
1
Reyommy :
barikiwa sana 🙏🙏
2026-05-23 15:32:52
1
user65154963888146 :
nikweli
2026-05-09 15:09:17
1
user654749484097 :
somo zuri❤️
2026-06-10 17:48:49
1
orestha forever :
noted
2026-05-14 18:13:43
1
Fania :
Asante kwa somo
2026-05-13 15:49:06
1
kipezya355 :
Kweli kabsa
2026-05-10 10:28:26
1
shijow :
umetisha
2026-05-21 11:25:19
1
Gee❣️ :
nimejifunza
2026-05-11 10:26:18
1
O💋💋&J❤❤ :
nimependa sana point zako mfanya biashara ukifata kama ulivoeleza utafika mbali sana ❤️❤️
2026-05-30 15:23:48
1
mima :
ni kweli kabisa kaka Asante kwa somo barikiwa sana
2026-05-08 20:04:57
5
juliana :
hakika
2026-05-10 08:42:06
1
mamacathe34 :
ndiooo
2026-05-13 10:09:12
1
ridhiwani mdoe :
hakika
2026-06-11 20:14:44
1
Prossy Nakamya :
good
2026-05-14 16:59:46
1
dams :
Sw mkuu
2026-06-07 15:59:36
1
samwel lukinda :
Kaka yote uliyoyasema yameua mtaji wangu haraka sana nilikuwa na zaid ya mtaji wa milioni 16 kwa sasa hali siyo poa nimeamua kujifunza zaid maana hilo ndo tatizo liloniweka pabaya🙏🙏🙏🙏
2026-06-11 11:13:08
1
Sophia Abdallah :
Kweli kbs
2026-05-16 07:27:13
1
nadhifa mohamed :
ahsante
2026-05-12 15:05:37
2
To see more videos from user @iem_pius, please go to the Tikwm
homepage.