@machingatvtz: MMILIKI wa kampuni ya Dr Toyota, bwana Salim Mbuma, amesimulia kisa cha kijana aliyempa kazi lakini baadaye akatoroka bila taarifa yoyote. Dr Toyota amesema tukio hilo limemsikitisha sana, akieleza kuwa baadhi ya vijana wamekuwa na tabia ya uvivu na kukosa uvumilivu katika kazi. Ameongeza kuwa mafanikio yanahitaji kujituma, nidhamu na subira badala ya kukata tamaa mapema. “Vijana wengi wanataka mafanikio ya haraka bila kupitia changamoto za kazi,” amesema Dr Toyota. Kauli yake imeibua mjadala mkubwa mtandaoni ambapo baadhi ya watu wameunga mkono maoni yake huku wengine wakisema mazingira ya kazi nayo yanapaswa kuangaliwa ili kuwafanya vijana wabaki kazini.
Kuna mambo mengi sana kwa vijana. Ila wakuu kuteseka sio sifa, kama mtu unaona kitu hakikufai achana nacho mapema sana sio kuwaza mambo ya job security. Ila ukiondoka aga
2026-05-12 19:26:38
276
Benson tz255 :
Mnaajiri matozi mabrotherman mapisi kali mnakuja kulalamikia vijana mnatukosea sana.
2026-05-13 06:44:54
184
Estro🦝 :
Maisha expensive ukileta uchumi tunasepa chapuu.Amna kazi yenye pay nzuri mtu akimbie bhn
2026-05-12 20:48:21
76
حمود :
vijana wanapenda kazi nyepesi
2026-05-12 18:40:33
27
bmtzappliances :
Vijana wanazinguwa sana 💔
2026-05-12 19:23:07
17
The shooter :
Kama sio wa kwanza kuacha fanya research shida ni nini hapo kazini kisha tuletee balanced story
2026-05-13 06:05:25
29
Zohain Faith :
Kazi tunafanya ila mnasumbua kwenye malipo
2026-05-13 04:10:42
29
Ammar :
Kwahio doctor toyota ulianza kaz ukiwa mzee sio
2026-05-13 07:09:20
27
kelvin_ :
Nina wazo ila kama nitalisema nitapingwa...
ila mi ninachojua organization/corporation yoyote inajali profit sanaa, wanaweza kuongeza au kupunguza wafanyakazi muda wowote. Issue ya mishahara na benefits kwa mfanyakazi huwa linawekwa kwenye kiwango ambacho hakiathiri faida ya boss....Kiufupi kampuni yoyote inajali faida zaidi kuliko chochote
2026-05-12 20:06:36
31
Ammar-AfroShiraz :
vijana wengi hawataki kuamini kwamba maisha ni process
2026-05-12 20:49:50
15
Holy_cakes_tz and more :
Asante doctor mi pia naajiri kwenye keki upuuzi kibao na wanataka maisha mazuri ,Ttzo hawajui ss maboss tulikuwa chin ya watu before na tulijiheshimu na kuvumilia sana ndio Mungu akatufikisha tulipo fika 🙏
2026-05-13 05:02:28
12
Vacation💵💵 :
kaka umesema ukweli yaan wanakuja kazin kama vacation
2026-05-12 19:17:34
26
Msomali furniture&home decor :
wanaishia kuwa kina Anko chai
2026-05-12 19:30:13
15
fixer mbega :
kujifunza kupo boss
2026-05-13 04:16:49
6
Hamza :
kaka nakuelewa saaanaaaa nipo Cape Town hapa nashughulika na construction eehh brother nina mwaka wa Tatu huu after lock down ya Corona aaah mzeee nimeamua kufanya kazi na wamalawi kaka wabongo Wana high expectations kaka
2026-05-12 18:56:44
35
DesignerMax :
kuteseka sio sifa boss
2026-05-12 20:08:11
25
King Hash :
wanapenda maisha rahisi
2026-05-12 19:27:30
7
Wa_Mipakani :
Hili ni janga la taifa aiseeeee
2026-05-12 18:18:08
10
DedeJr :
kweli bro wanadengua sana madogo
2026-05-12 19:22:41
6
Part Kamba :
Sio kwel
2026-05-12 18:53:04
8
MindCove. :
huyo alikuwa sio mfanyaji kazi maana alikuwa anatamaa tuu
2026-05-12 19:11:13
8
Frank :
hata Mimi nimeacha kazi Sana mpaka 35yrs. siku hizi nimetulia.
2026-05-13 06:27:11
6
kenzo gear :
wenye uitaji tupo
2026-06-08 06:31:06
1
To see more videos from user @machingatvtz, please go to the Tikwm
homepage.