@kingdaddytz: TOFAUTI YA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA NI HIZI. Yanga uwanjani hawafiki ni wavivu tena timu ikiwa inafanya vizuri ndo kabsaaaa hawajitokezi kwa wingi sio Kimataifa wala mechi za ndani. Simba wala huhitaji nguvu kubwa kuwaambia twendeni kuishangilia timu their always there kwaajili ya timu yao pendwa nadhani ile NGUVU moja huwa wanai upply hapo. Yanga wana Misimamo mikali sana hasa ukipishana nao kwa namna yeyote ile ku turn na kuwa adui yao ni Asubuhi tu yani. Wana kiburi fulani cha kihehe cha " tunashida ndio ila hatukutaki wewe" tena issue ikiwahusisha wazee wa yangasc aaah hiyo kuamuliwa labda ichinjwe Ngamia . Si unaona kama wanavompepelea GSM na ENG Hers sasa hivi siku wakimgeuka hutaweza hata kudhani waliwahi kumbeba kwenye kiti kama MUTWA wa wahehe. Simba wao huko kwenye kuwa na msimamo ni wachanga bado, mfano miezi kadhaa iliyopita kuna akidi iliitisha press kuwa hawamtaki Mo dewj lakini wakafurushwa kama Kenge mla kuku mtaani then kimyaaaaa wananung'unikia shingoni. Issue kama ile ingetokea kwa Yanga weeee pasingetulia kirahisi bila kuanguka mbuyu chini. Simba kwenye masuala ya kusaidia timu kwenye michango mbali mbali huwa wana roho za Kipare sana ubinafsi na kuamini kuna wanaotakiwa kuisaidia timu wao kazi yao ni kwenda kushangilia na kuzomea uwanjani tu. Yanga hakuna kitu wanakipenda kama kuchangia timu na ukitaka wajae uwanjani waambie kutakua na bakuli la kumchangia mchezaji au kiongozi weeee wanajaa mpaka unashangaa huu ujamaa wameutoa wapi..?? Simba kuwapa wachezaji maokoto tu huwa ni mzozo sana ila watani zao kule mtu kuokoteshwa million 10 ni issue ya kawaida. Kuna namna Yanga wanatakiwa kujifunza jinsi ya kuisupport timu yao kwa kufika kwa wingi uwanjani inapohitajika Waache ushua mpira unahitaji mashabiki vichaa uwanjani wafia timu. Simba kuna la kujifunza kwa Yanga kwenye kuwajibikia changamoto za Timu yao kujaa tu uwanjani huku roho zimejaa ubahili ndio sababu wanasikitikia ndani kwa ndani hatumtaki fulani wakisogezewa mic waseme wanakua bubu. Yanga ni kama wanapenda shida zaidi kuliko Raha. Wanakuja viwanjani kwa kujivuta wanatoa sana michango na kujisajili. Simba wanapenda raha zaidi ila hawako tayari kushiriki kuzitengeneza. Sasa sijui nani bora wanaokuja uwanjani kuipigania timu kama mchezaji wa 12 uwanjani au hawa wazee wa harakati nyingi kuja uwanjani hamna kitu. Anyway TUKO MUHEMI TUNASIKILIZA RADIO MBAO. Full story tembelea youtube pale MNYALUKOLO ONLINE MEDIA. . . . . . #tiktokmichezo🇹🇿🇹🇿 #uchambuziligikuutanzania #Uchambuzi #simbavsYanga #sportsontiktok