@chawamata_tv: VIDEO: Mbunge wa Jimbo la Mlalo kupitia chama cha CCM, Rashidi Shangazi, amesema madereva wengi wa malori nchini wanaofanya kazi ya kusafirisha mizigo hawana mikataba rasmi ya ajira, hali ambayo inawanyima uwezo wa kutetea maslahi yao wanapokumbana na changamoto kazini. Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi bungeni, Shangazi amesema madereva hao husafirisha mizigo yenye thamani kubwa kutoka bandarini kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini bado hawapati stahiki zao za msingi kutokana na kukosekana kwa mikataba ya kazi. Amesema kukosekana kwa mfumo rasmi wa ajira kwa madereva hao kunaikosesha hata Serikali mapato ya kodi kwa sababu wengi wao wanakuwa hawatambuliki rasmi kwenye mifumo ya ajira na kodi. Mbunge huyo ameishauri Land Transport Regulatory Authority pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kukaa pamoja na kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu changamoto hiyo ili madereva waweze kutambulika rasmi na kulindwa kisheria. Katika hatua nyingine, Shangazi amehoji gharama wanazobeba madereva ili kupata sifa za kuendesha malori makubwa, akieleza kuwa ili dereva aweze kupata leseni ya daraja E analazimika kuwa na daraja C pamoja na kuhudhuria mafunzo maalum kwa muda wa siku 14. Amesema mafunzo hayo yanahitaji dereva kulipa takribani shilingi laki tatu, jambo ambalo limekuwa gumu kwa wengi wao kutokana na kutokuwa na ajira rasmi wala mishahara ya uhakika. “Dereva huyu hana mkataba wa kazi, hana mshahara wa uhakika, anatakiwa kukaa darasani siku 14 na bado alipe shilingi laki tatu. Fedha hizo atazitoa wapi?” amehoji Shangazi bungeni. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #MediaTanzania #OnlineTV #TrendingTZ #TanzaniaTrending #ViralTZ #TeamChawamata #SupportLocal #MadeInTanzania #RoadTo100K #tanzaniatiktok

CHAWAMATA TV
CHAWAMATA TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 13 May 2026 11:32:06 GMT
229979
12945
787
1303

Music

Download

Comments

isihakawandi
isihakawandi :
madereva tu comment kwa wingi
2026-05-13 13:49:30
187
golden.boy5443
golden boy :
mungu watunze watu kama awa madereva wote tuseme amen 🙏
2026-05-13 18:55:26
67
salimsheikhmbwana
salimsheikhmbwana :
Mungu akutunze Mkuu utusimamie kwenye hili janga lakitaifa
2026-05-13 12:12:52
66
user405691379308
user405691379308 :
Hakika mungu humsikia hata bubu asiyeweza kuongea nahc na naamini kuwa Wakutusemea tumempata Mungu tulindie huyu mtu.Amiin🙏🙏🙏
2026-05-13 16:21:50
34
mtaya.silaju
Mtaya Silaju :
mungu akubark Kila upande
2026-05-13 13:31:29
16
marlaw35
Marlaw :
Shukrani sana kwa huyu mbunge madereva niwatu wa maana sana lakini tunachukuliwa kama watu bure hatuna maana
2026-05-14 06:26:43
13
wiliammboya
Wiliam Mboya :
Bora utusaidie kuongelea hilo Asante sana
2026-05-13 12:33:43
20
barakatz75
B:R"K🚛 :
asante sana tumepata wakutusemea daah mwenyezi mungu abaliki hili jambo 🙏🙏
2026-05-13 21:17:48
12
ramaomary978
Rama PUTINi 🇷🇺🎯 :
I ihii ni ndoto au . maana tumepata msemaji leo Bungeni. GOD BLESS ANKO
2026-05-13 13:45:12
15
godfreymartin323gm
[email protected] :
mzee apo umefanya lamaana sana
2026-05-13 17:16:01
6
vanstrm3
Evans tarmo :
wakat wa mungu umetufikia madereva
2026-05-13 16:19:40
6
sittathomas451
sina maana hiyo :
shukrani sana mkuu kwa kututetea maana tunanyanyaswa sana
2026-05-16 11:15:35
7
kulwampela
MPELA :
TUNASHUKULU kwakutukumbuka
2026-05-13 18:22:05
5
zamil.samir
Zamil Samir :
asnte mkuu rashid s mungu akuweke
2026-05-13 17:42:42
8
user9787252142271
ally hamis :
mungu ukulinde mbunge uzid kututetea
2026-05-14 04:20:59
5
user2513617292526
user2513617292526 :
Ahsante cna mkuu Kwa kutusemea mungu akulinde cku zote,
2026-05-13 21:03:07
5
abuubakari705
Abuu :
ni kweli hilo swala madereva wengi tunafanya kazi bila mikataba
2026-05-14 08:12:09
5
lone.survivor57
lone survivor :
point sana mkuuu umeongea masharti kibao lkn Kaz mbovu
2026-05-13 18:10:15
5
liberatidamas
liberatidamas :
sio siku 14 kiongozi ni mwezi saiv
2026-05-13 13:19:26
8
user1659123263659
user1659123263659 :
Ongeza na 20000 kwa ajili ya LATRA
2026-05-13 13:01:28
7
nashirukasongo
nash k :
Asante sana serikali imetudisha nyuma nimesoma nit psv nimeenda kulinyuu wamekata class E .sento mpaka nikasome na kazi cna
2026-06-19 12:51:04
0
baracka.mboje
BMM 🇹🇿 🇹🇿 🇹🇿 :
jamani tumeonekana na sisi 👍👍👍
2026-06-17 17:33:17
2
...najmah
NAJMA🦋 :
Nimefurah sana🙏
2026-06-18 14:21:25
2
justinemarolasa
JustineMarolasa🇹🇿 :
ishi sana kiongozi 💪
2026-05-16 13:47:15
2
athumanimakwogo
Athuman :
asante sana mkuu
2026-05-14 06:24:53
1
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About