@healthyfity1: Ushawahi kukutana na hali ya mishipa ya shingoni kuvimba hivi? Severe tricuspid regurgitation inaweza kuwa moja ya sababu zinazoweza kusababisha Jugular Venous Distension (JVD). Hii ni hali ambapo valve ya upande wa kulia wa moyo (tricuspid valve) haifungi vizuri, hivyo damu hurudi nyuma badala ya kwenda mbele kawaida. Hali hiyo huongeza presha kwenye mishipa ya damu ya shingoni, ndipo mishipa huonekana kuvimba au kusimama wazi. Dalili zinazoweza kuonekana: • Mishipa ya shingoni kuvimba (JVD) • Miguu kuvimba • Kuchoka haraka • Kupumua kwa shida • Mapigo ya moyo kwenda tofauti wakati mwingine Hali hii huhitaji uchunguzi wa daktari wa moyo kama vile: • Echocardiogram (ultrasound ya moyo) • ECG • Vipimo vya damu na uchunguzi mwingine wa moyo