@wajanjaforum: Sio kila jina la urithi ni baraka… majina mengine hubeba historia nzito kuliko tunavyodhani. Kuna familia zinaendeleza majina ya ukoo bila kuuliza: huyu mtu aliishije? Aliacha historia gani? Alibeba baraka au mizigo? Wazee walisema jina lina nguvu, na kabla hujamwita mtoto jina la babu au bibi, chunguza vizuri maana yake na historia yake. Usibebe kila kitu kwa kisingizio cha utamaduni. Chagua jina lenye baraka, maana jina linaweza kuwa mwanzo wa hatima. Je unaamini majina yanaweza kuathiri maisha ya mtu? 👇 #MajinaNaHatima #SimuliziZaWazee #UkooNaHistoria #MaishaNaSiri #BarakaZaFamilia #TanzaniaReels #SwahiliReels #MamboYaKiroho #HadithiZaUswahilini #JinaLinaNguvu