@kulwa2712: Kwa mama mjamzito, vyakula hivi vina faida nyingi sana kwa afya yako na ukuaji wa mtoto tumboni: MAYAI YA KUCHEMSHA Faida zake: ➡️Husaidia kujenga mwili wa mtoto tumboni kutokana na protini nyingi ➡️Yana choline ambayo husaidia ukuaji wa ubongo wa mtoto ➡️Husaidia mama kupata nguvu na kupunguza uchovu ➡️Husaidia mifupa kuwa imara kutokana na vitamini D TANGO Faida zake: ➡️Lina maji mengi hivyo husaidia mwili kuwa na maji ya kutosha ➡️Husaidia kupunguza kuvimba mwilini kwa baadhi ya wajawazito ➡️Husaidia mmeng’enyo wa chakula na kupunguza choo kigumu VIAZI VITAMU ➡️Vina vitamin A inayosaidia ukuaji wa macho na kinga ya mtoto ➡️Husaidia mmeng’enyo mzuri wa chakula kutokana na nyuzinyuzi. Kwa mama mjamzito, kula vyakula hivi kwa pamoja asubuhi inaweza kuwa kifungua kinywa kizuri na chenye afya sana.

Afya uzazi clinic
Afya uzazi clinic
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 26 May 2026 07:27:41 GMT
17893
278
1
5

Music

Download

Comments

malick079
Gerlany fashion enfants🇨🇩✌️ :
❤️❤️❤️
2026-06-07 03:37:04
0
To see more videos from user @kulwa2712, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About