@atuganilemwakosya: Maelfu ya watu wakusanyika kwenye mkutano mkubwa wa Injili nchini Netherlands ambapo mamia kwa maelfu walimgeukia Kristo huku wengine wakibatizwa hadharani kama ishara ya kuanza maisha mapya ya wokovu. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, inakadiriwa zaidi ya watu 60,000 walihudhuria mkutano huo mkubwa uliogubikwa na maombi, ibada na mahubiri ya Injili yaliyowagusa wengi. Mashuhuda wa tukio hilo walisema nguvu ya Mungu ilidhihirika kwa namna ya kipekee huku watu wengi wakionesha kuguswa kiroho, kutubu dhambi zao na kuamua kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. #missionistomakejesusfamous #ToGodBeAllTheGlory #FollowJesus #ChristianNews #jesuscomingsoon