@selemanisogo72: Bro, umri wa miaka 25-30 sio umri wa kufanya mzaha. Si umri wa kula ujana. Ni kipindi ambacho maisha yanaacha kukulaghai na yanaanza kukuonyesha ukweli. Kati ya miaka 25–30, reality inapiga kwa nguvu. Unaamka na kugundua muda haupo tena. Unaanza kuhesabu miaka badala ya ndoto zako. Unatazama watu wanaendelea, halafu wewe unahisi bado upo nyuma. Cha uchungu unakuzidi zaidi,, kama mwanaume, hakuna watu wengi wanaosimama kusikiliza matatizo yako. Watu wanatarajia ujipange mwenyewe. Ndiyo maana unabeba maumivu na presha Yako kimya kimya. • Presha ya kufanikiwa. • Presha ya kutafuta pesa. • Presha ya kusaidia familia. • Presha ya kuwa “mtu fulani”. Ndani yako unajiuliza: “Nimefail wapi?” “Nilipoteza miaka yangu bora?” “Mambo yatabadilika kweli?” Bro, nikwambie ukweli; hiki kipindi hakijatengenezwa kuwa faraja. Kimetengenezwa ili ujijenge kupitia maumivu, kukataliwa, kufukuzwa na kuumia zaidi. Hapa ndipo wavulana wanakuwa wanaume, au wanabaki wavulana milele. 🕒 1. Kubali Ukweli: Muda Haukusubiri. Muda hautosimama kwa sababu unaogopa, umechanganyikiwa au maisha hayakuwa fair. Kila mwaka unaochelewesha kuchukua hatua, unaulipa kwa majuto. Huu sio msimu wa kufuata starehe. Ni msimu wa kufuata mwelekeo wako wa maisha. ❤️ 2. Usifanye Mapenzi Kuwa Suluhisho. Acha kufukuzia wanawake kama ndiyo jibu la maisha. Mapenzi ni mazuri, ndiyo, lakini: • Mapenzi bila uthabiti yanakumaliza. • Mapenzi bila lengo yanakupoteza. • Mapenzi bila kukua kifedha yanakuvunja. Mwanamke anaweza kukaa na wewe ukiwa una pesa, lakini heshima hupungua pale maendeleo yanaposimama. Huhitaji kuwa tajiri leo, lakini onyesha jitihada, dira, na ukuaji. Epuka wanawake wa kudai tu: muda wako, pesa, attention. Wanakuchosha akili na mifuko yako. Mwanamke wa kujenga naye maisha analeta amani, sio presha. Analeta Msaada, sio stress. 💰 3. Jifunze Kuhusu Pesa Mapema. Pesa hazikupi furaha, lakini kukosa pesa kunakunyenyekeza vibaya. Jifunze jinsi pesa inavyofanya kazi, hata kama ni ndogo. Pesa ndogo hufundisha nidhamu, subira na control. Acha kutumia pesa kuonyesha watu. Acha kununua vitu usivyohitaji ili kufurahisha watu ambao hawatakusimamia siku maisha yatakapokupiga. Wekeza kwenye skills. Jifunze kitu chenye thamani online au offline. Skill itakupa confidence ambayo pesa peke yake haiwezi. 🚫 4. Ua Addiction zako Mapema. 🫴🏾Pombe. 🫴🏾Dawa za kulevya. 🫴🏾Porn. 🫴🏾Kamari. 🫴🏾Party zisizoisha. Havikupumzishi bali vinakuchelewesha. Vinaiba focus. Vinamaliza nguvu. Vinaufanya wastani uonekane sawa. Mwanaume asiyeweza kujidhibiti hawezi kudhibiti future yake. 🙏 5. Rudi Kwa MUNGU kwa Dhati. Usimtafute Mungu pale tu mambo yakiharibika. Mfanye awe msingi wako. Omba hekima, si pesa tu. Omba nidhamu, si baraka tu. Muamini Mungu lakini fanya kazi kwa bidii. Imani bila juhudi ni matumaini tu. 🧠 6. Usikate Tamaa. Ni sawa kulia. Ni sawa kuchoka. Ni sawa kukata tamaa kwa muda. Lakini elewa hili: huna option ya kuacha. Kama mwanaume, hakuna mtu anayekuja kukuokoa. Maumivu yako ni Siri. Lakini mafanikio yako yatawabeba wengi. Acha kutangaza mipango yako. Anza kimya kimya. Acha Matokeo ndiyo yapige kelele. ✅ HITIMISHO. Kati ya sasa na mwisho wa 2026, maisha yako yanaweza kubadilika kabisa. Si kwa motivation. Si kwa kutamani. Lakini kwa: nidhamu, consistency, na sacrifice. Siku moja utakaa chini useme: “Ilikuwa upweke. Ilikuwa ngumu. Lakini sikukata tamaa.” Na siku hiyo Bro, utaelewa kwa ni kipindi kilichokuwa muhimu sana. 👉 Share hii post kwa mwanaume unayejali. 👉 Nifollow kwa mada zaidi za maisha na mahusiano. #selemanisogo72 #MotivationTZ #DisciplineMindset #KenyaTikTok #FYP2026
@sogo72
Region: TZ
Wednesday 27 May 2026 08:13:02 GMT
Music
Download
Comments
marwapeter60 :
bro mungu akupe uhai maana nimejifuza kitu 👏👏👏
2026-07-02 15:49:00
4
Erick Shayo :
bro, bro,bro, nimekuita mara tatu Mungu akubariki
2026-07-04 22:19:51
3
F.Crawford@🇨🇩 :
daaaah kwelii kak
2026-06-12 17:16:28
2
West Man :
2026-05-31 12:28:50
2
Ashfak Ab :
Shukran sana kaka pia kama hutojali ningependa hili andiko lako niweze kupata nafasi ya kulidownload ili niwe nalisoma kila ninapohisi kushindwa
2026-06-12 16:54:29
3
Chidymomo_tz :
Umenigusa sana
2026-05-31 05:25:02
1
Keddy p :
daaaah point sanaaa
2026-05-31 17:40:45
1
WISO✌️ :
Kaka hii imenigusa Sana 🙌 barikiwa mnoo
2026-06-01 08:57:10
1
01_maysix :
💯 great advice mkuu
2026-06-05 19:43:09
2
Joel Morgan :
bro hayo yote naona yananihusu mm thanks Sana bro
2026-05-31 09:22:28
15
mayala junior :
sjawahi kucoment leo nasema ahsante sana mungu akubariki
2026-05-31 09:27:37
8
BIN ABEID :
asnte nimeona na ndio yanyopitia mikononi mwetu
2026-06-11 15:01:03
2
PERFECTCRISPIN🌏 :
sio poa kabisa 🙌🙌
2026-05-31 09:41:06
1
Ashelly Meshack :
Amini kaka
2026-05-31 10:41:41
1
RAM🎧DIZOOH 🎶 :
ushauri mzuri sana💯
2026-06-13 10:00:06
2
gerrad philimon :
mungu akupe maisha malefu kaka
2026-06-11 22:04:39
3
Meddy :
respect kwako kiongozi
2026-06-11 12:22:54
3
January Samwel :
Kubwa sana 📌
2026-05-31 04:36:40
1
dady.lee :
blessed 🙏
2026-05-31 08:41:41
2
ÄẀÜŒĤ :
dah...wengine ni God tu atujalie ...tumejaribu na tutazidi kujaribu 🙏🙏🙏🙏🙏🙏
2026-05-31 20:48:40
4
anord pallanjo :
aseee sio poa hpa umenifanya niwe shujaaa
2026-05-31 17:27:09
1
Ally Ladies Store :
Respect Mzee kwa heshima 💪
2026-06-01 19:23:35
3
Issa Mohamed :
og🙏
2026-05-31 02:08:07
1
bonninho27.."# :
you got me broo
2026-05-27 17:47:04
1
OMY OMY :
dah! bro
2026-05-27 11:31:27
1
To see more videos from user @selemanisogo72, please go to the Tikwm
homepage.