@evanjelistsarahodero: MAOMBI YA ASUBUHI Baba nakushukuru kwa wema na fadhili zako kutufikisha siku ingine na asubuhi nyingine ya Baraka maana si kwa uweza wetu bali kwa uweza wako! Imeandikwa mshukuruni Bwana kwa kuwa yu Mwema maana fadhili zake ni za milele nasi Tunakushukuru kwa maana fadhili zako ni za milele eeh Bwana Mungu wetu! Ni Asubuhi ya kutamka tunachohitaji mbele zako eeh Bwana Mungu maana Imeandikwa kwamba ombeni nanyi mtapewa nasi twaomba na kutamka ili tupokee ushindi kwako ndani ya siku hii ya LEO! Natamka kwa mpendwa huyu akapokee kibali na ushindi siku ya leo,kila hitaji analohitaji akalifanikishe kwa jina la Yesu Kristo aliehai,Imeandikwa pia Baraka ni haki yetu nami Natamka Baraka ikawepo juu yake akainuliwe kiuchumi kupitia jina la Yesu Kristo aliehai. Tunakwenda kinyume na kila mpango wa ibilisi Imeandikwa mwana wa Mungu amedhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi, nasi tunazivunja sasa kwa mamlaka ya jina la Yesu Kristo aliehai. Adui alietega mitego yake ya kichawi kwenye ofisi yako leo tunategua na kusambaratisha kwa mamlaka ya jina la Yesu Kristo aliehai. Natamka ushindi juu yako mpendwa Pokeaaaaa afya njema na ukastawi sasa maana Imeandikwa nitakurudishia afya yako na kukuponya ndivyo asemavyo Bwana wa majeshi nasi twasema Pokeaaaaa afya njema kwa Damu ya YESU na siku ya LEO ikawe ya Amani kwako maana pia Imeandikwa kwamba Yesu Kristo ni mfalme wa Amani na iyo Amani ikatawale kwa familia yako na maisha yako Katika jina la Yesu Kristo aliehai Ameeeeeeeeen UBARIKIWE SANA,, #fyp #amen