@adv.witness: Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, chini ya vifungu vya 69, 70 na 71, sheria inatambua ahadi ya ndoa pamoja na mali au matumizi yaliyofanywa kwa matarajio ya ndoa kufungwa. Aidha, madai ya uvunjifu wa ahadi ya ndoa yanapaswa kufunguliwa ndani ya mwaka mmoja tangu uvunjifu huo ulipotokea. Katika kesi ya Anna Mgamba v Mathayo Msigwa [2022] TZHC 10229, Mathayo alidai kuwa alitumia fedha kujenga nyumba baada ya kupewa ahadi ya ndoa. Ndoa haikufungwa, na mahakama iliridhika kuwa matumizi hayo yalifanywa kwa matarajio ya ndoa iliyotarajiwa kufungwa. Rufani ya Anna Mgamba ilitupiliwa mbali. Ahadi ya ndoa si lazima iwe ya maandishi. Mahakama inaweza kuangalia mazingira na mwenendo wa wahusika ili kubaini ukweli wa jambo. // Under Sections 69, 70 and 71 of the Law of Marriage Act, 1971, the law recognizes promises to marry and property or expenses incurred in contemplation of marriage. The law also requires an action for breach of promise to marry to be brought within one year from the date of the breach. In Anna Mgamba v Mathayo Msigwa [2022] TZHC 10229, Mathayo claimed that he spent money constructing a house after being promised marriage. The marriage never took place, and the Court was satisfied that the expenditure had been incurred in contemplation of the intended marriage. Anna Mgamba’s appeal was dismissed. A promise to marry does not necessarily have to be in writing. The Court may consider the conduct of the parties and surrounding circumstances in determining whether such a promise existed. #SheriaImerahisishwa #LawMadeEasy #AquilaAttorneys #AdvWitness #SheriaYaNdoa
Adv. Witness
Region: TZ
Friday 29 May 2026 16:50:54 GMT
Music
Download
Comments
Ngichunguria :
Watz wameamka mambo haya ilikuwa kesi nyingi za nje❤️...hongera Wakili Msomi kwa elimu
2026-05-29 17:56:00
9
Heri Zachariah :
sawa vizuri, lakini kuna nyumba ya sh mil 3.87?
2026-05-30 02:54:34
4
AGIZA BIDHAA DUBAI :
Uko makini sana🥰
2026-06-03 16:42:25
1
Blessed Mtey :
Wakili Msomi. Kazi yako ni njema sana. Mungu Akubariki sana
2026-05-30 18:37:24
4
kayo boy :
dada unajua napata darasa
2026-05-30 15:22:01
2
SHAFIYU :
mashallah hongera wakili
2026-06-06 13:26:22
1
Mr KAMODO :
naomba kujua, je mahakama inaeza kuangalia maswala ya mahali ili kusuruhusha mambo ya watoto wabaki na mama au baba?
2026-06-01 17:29:47
0
SATIVA 6767 :
mbn wakili ni mzuri kuliko hta huyo anna🥰
2026-06-02 06:33:55
4
Emmashev :
Asante sana 🙏
2026-05-29 21:47:16
0
Aggyie :
wakili msomi, good
2026-05-29 20:29:53
1
Sarah_ :
Mamaaaaaa😁
2026-05-29 21:21:30
0
johary🦋❤️🦋❤️ :
barikiawa sana kws elimu🥰
2026-06-02 02:51:20
0
Diana living :
Naomba kukupigia 👏
2026-06-02 20:42:35
0
phinah :
unasauti nzuri kipenzi
2026-05-30 14:49:00
0
HUDUMA ERRANDS TZ :
big up ccy 👏❤️
2026-05-29 16:55:08
0
msafiriharidi :
hiyo nzuri
2026-05-29 17:32:28
0
kimaro Tz :
nakukubali sana madam umekuwa msaada
2026-05-29 17:35:35
0
Dr.Mussa :
nimeipenda hiyo
2026-05-29 17:57:27
0
idriss :
i found this useful😊
2026-06-05 22:43:23
0
user5629146467880 :
Thanks Advocate.
2026-06-03 21:10:27
0
SH4F11 :
mmmmh ILA ANNA !
2026-06-06 10:45:42
0
Jay Mombasa :
ilikua ni nyumba gani hiyo ya million 3 za Tanzania! hata room moja na sitting room hazijengi
2026-06-07 04:43:36
0
Ellison :
muda wa kupata darasa🔥
2026-05-30 06:17:15
0
Sam :
Umeeleweka, good
2026-05-31 09:18:30
0
Amose Wema :
nakufuatilia sana sanaa una kitu, kwanza umeweza kutoa sheria kingereza kuja kiswahili big up sana, usiache
2026-06-01 16:58:38
0
To see more videos from user @adv.witness, please go to the Tikwm
homepage.