@the.syntrix.nuru: Simu haijaiba muda wako kwa ghafla. Inaiba maisha yako kidogo kidogo kila siku. Kila ukimya unajazwa na scrolling. Kila boredom inaondolewa na videos. Kila dakika ya kufikiri imechukuliwa na notifications. Watu wengi siku hizi wako active sana online… lakini hawapo present kwenye maisha yao halisi. Wanashindwa kula bila simu. Kulala bila simu. Kutembea bila earphones na scrolling. Hata kuongea na mtu uso kwa uso attention yote ipo kwenye screen. Tatizo sio simu kuwa mbaya. Tatizo ni pale unaposhindwa ku-control matumizi yake. Attention yako ndiyo nguvu yako kubwa. Na dunia ya sasa inapigania attention yako kila sekunde. Kadri unavyozoea distractions, ndivyo akili yako inavyozidi kupoteza uwezo wa kutulia, kufikiri kwa kina, na kuwa focused. Jaribu hata dakika 30 kwa siku bila simu. Utashangaa akili yako inaanza kutulia tena. Unaanza kuona maisha vizuri zaidi. Unaanza kuwa present kwenye moment badala ya kuishi kupitia screen. #mindset #SelfImprovement #focus #discipline #growthmindset