@tok.bnez: Watu wengi huzaliwa familia ambazo hazikuweka RAMANI ya mtoto huyo husika anakuja kufanya nini duniani. Watoto “walitengenezwa” kwa EXCITEMENT YA SEX au by “HAPPENSTANCE” au kwa kelele za UKWENI au hata kwa mashindano nani mke wake wake ana “KIZAZI” kinachofanya kazi. Ndo maana hata MAJINA wanayopewa watoto wengi ni majina ya kimazoea tu. Hayaonyeshi PURPOSE ya huyo binadamu kuja duniani. Either ni majina ya kidini tu yaani “GOOD LUCK NAMES”. Au majina ya kimazoea tu. Sijui kama wewe Wazazi walikwambia walikuzaa uje ufanye nini? Did they? Na jina lako uliambiwa PURPOSE BEHIND au ndo jina la bibi au babu au jina tu la “kizungu”🤷🏽‍♂️ Kwa hiyo kuanzia kuja kwake mtu duniani ilikuwa ni WATU TU WANAONGEZA FAMILIA au basi ILITOKEA TU hivyo mtoto ndo yupo. Hakuna PURPOSE nyuma ya huyo mtoto wala wazazi hawakai kuiwaza sasa kuwa sasa mtoto yupo okay tumuandae kuwa alichokusudia Mungu. Wazazi discussion yao kubwa ni mahitaji BASIC ya mtoto nguo, chakula, matibabu akiumwa, ada akikuakua. Period. Imagine umetoka mazingira hayo. Hata wewe hujui ulikuja duniani kufanya nini. Hivyo UNAZURURA TU. Na kwenye kuzurura kuna watu wameajiriwa sehemu ambayo hawakupaswa kuwa. Zinawapa pesa Ila haziwapi FULFILMENT. Wanazurura. Kuna watu wanafanya BIASHARA kama mkumbo. Hataki kujua hivi ni biashara gani itanisaidia TO BE A BETTER VERSION OF MYSELF. Hivyo atafanya hata haramu. Atauza hata vitu vinavyoharibu AFYA ZA WATU AU ROHO ZAO kwa sababu yuko so focused na PESA tu na si kujua duniani alikuja kufanya nini. Namna mojawapo ya kujua nini uliumbwa kufanya hapa duniani ni: 1. Removing the MONEY FACTOR. Jiulize. Hapo ulipoajiriwa hiyo kazi unayofanya au biashara kama ungepewa tu nauli unaweza kufanya BURE? Ukiona jibu ni HAPANA kwamba sasa nitaishije? Jua tu hapo ulipo hiyo SI CALLING YAKO! Upo ili kutimizia majukumu yako. The idea siyo kufanya BURE the idea ni kutrigger mind yako kuwaza CAN I DO THIS FOR FREE? Pesa ni muhimu tena SANA MNO MNO niamini nachosema… lakini ni nzuri zaidi ukiwa unaipata ukiwa FULFILLED.. Watu wengi wanafanya kazi vitu ambavyo ni Wazazi walimsomesha kwa influence yao. Wazazi wanaweza kukuuzia DREAM ZAO na ukaamini ni zako. Watu wengi wanafanya biashara kwa INTEREST tu. Siyo CALLING yake. Ukiona unaanza biashara unaacha hilo eneo si lako. Eneo uliloitiwa utaona lina tick a lot of boxes ndo maana huwezi kuacha mpaka wateja watakuja tu na mpaka brand itajengeka tu. Hili ni muhimu sana. CAN YOU DO WHAT YOU DO FOR FREE? Kama jibu ni HAPANA be SMART EARLY. 2. ⁠Jambo jingine litakalokusaidia kujua DUNIANI UNAPASWA KUSIMAMA WAPI ni kwa ku PAY attention kwa vitu ambavyo watu tofauti tofauti (wasiofahamiana) wanakwambia mara kwa mara kuwa UNAWEZA SANA. Do not ignore. VOXI POPULI VOXI DEI. The voice of the people is THE VOICE OF GOD. 3. ⁠Kitu kingine ni observe ni kitu gani ukikosea unaona “umezingua” sana na pia kitu gani unahisi unahitaji KUJIPANGA SANA ili ukifanye. Mara nyingi CALLING YAKO iko kwenye weakness zako. Musa aliitwa kuongoza taifa Ila alikuwa na KIGUGUMIZI PLUS HASIRA fikiria huyo ndo anatumwa kwa Farao. Angalia wewe kama una idea na unaiogopa ila kila wakati inakuja tu AMINI USIAMINI KWENYE HOFU YAKO NA WEAKNESS ZAKO NA IMPEDIMENTS ZAKO NDIPO ILIPO CALLING YAKO. Jump on that cliff. God will give you wings! 4. ⁠Tafuta pia vitabu hivi: THE ALCHEMIST, THE PURPOSE DRIVEN LIFE na THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI mimi hivi vilinisaidia mno nilipokuwa MWAJIRIWA karibu miaka 20 iliyopita. Go read them. Usiogope KUTHUBUTU vitu. Jump off the cliff. MBINGU zitakutunza. Zilitutunza sisi. Just BELIEVE. And jump off the plane ✈️ THE “PARACHUTE” 🪂 will work. If it doesn’t well at least you tried. Na ATAKUAGUZIA MALAIKA kweli na hutaaibika. Kuna watu wengi mno duniani wana suffer kwa sababu wewe hujaamua kusimama ULIPOPASWA KUSIMAMA KISA TU HUONI KAMA PANA HELA KWANZA. Start now. Usikubali kuwa MISPLACED. FULFILLMENT IS THE NAME OF THE GAME. Biblia inasema HERI MWISHO WA NENO (JAMBO) KULIKO MWANZO WAKE. Memento Mori, Semper Fi, Mr. Muhozya

Talk Business
Talk Business
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 01 June 2026 07:44:41 GMT
12194
1531
31
70

Music

Download

Comments

frida.gabriel7
Frida Gabriel :
That's very deep I wish everyone should not only listen but understand....And "The purpose driven Life book" has changed my life for good
2026-06-22 07:08:46
2
kyunyujumbe
kyunyujumbe :
“For where your treasure is, there your heart will be also.” Matthew 6:21
2026-06-01 12:58:10
6
kevin.mwemezi
Kevin Mwemezi :
Mungu akubariki sana
2026-06-10 04:39:21
1
callmehappy58
Ms HappY♡ :
kuwa misspleaced ni kunatutesa watu wengu mungu nipe nguvu ya kujua ipi ipi☺️
2026-06-03 01:57:19
4
tinnah.bel
Teeny❤️ :
I needed this Sir…thank yu so much
2026-06-01 09:39:15
2
joe_albaa
jøeAlßa :
mtoa madini🙏🙌
2026-06-01 08:46:24
3
joseph.ndongo15
Joe chazz :
Leo nimekuelewa
2026-06-17 11:06:46
1
kojodibo93
kossam :
cool
2026-07-01 06:34:31
1
shuntah2
@Shuntah :
Mimi huwa naelewa sana ushauri wako....keep it up
2026-06-19 22:04:11
3
user5833681075058
Lucky G (257) :
Tnk u
2026-06-08 09:43:51
1
dommy0935
dommy :
Kaka barikiwa sana
2026-06-23 16:47:50
1
madam.anna2
BINT SAYUNI 🥰 :
BARIKKWA BABA🙏
2026-06-22 11:50:45
0
user1087425600900
Anithamahaba :
Ahaaaaa kiongozi asante mm nilianza kazi ninayofanya kwa stress sababu kwanza nilikuwa siijui pili ni mbali tatu maadui wasiotaka niweze kufanya ni wengii but nilikomaa hv tunavyoongea kuna ambao wanashangaa nikiwezajee,lkn asikuambie mtu Mungu na focus umemaliza.Bila kusahau hilii majaribu yapo mpk sasa napita lkn ninaamin ktk utetezi wa Mbingu hata hili nitashinda🥂.SEE YOU AT THE TOP🙏
2026-06-29 13:06:36
2
jeanbisheni1
jean bisheni :
natamani ku funzwa mwalimu
2026-06-03 17:31:32
1
jaydenjackson348
Jayden🌱 :
Hili somo ni muhimu sana kwa Kila binadamu nataman limfikie Kila mtu
2026-06-01 14:46:44
2
nova.outfit2
nova_outfit :
🙏
2026-06-01 08:18:54
1
user2349758325507
samwel_ngulk :
🙏🙏🙏
2026-06-01 08:23:17
1
clearihb86r
Clear :
🧠
2026-06-07 09:34:34
0
tiktok.comuser4290
Katoto smart collection❤️🥿🥰 :
🥰🥰🥰
2026-06-10 13:27:48
1
packitbyangie
Packitbyangie :
👏
2026-06-02 05:17:46
0
To see more videos from user @tok.bnez, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About