@kidotty_bby: OMBEA MAHUSIANO YENU MUNGU AWAPE KIBALI CHA KUINGIA KWENYE NDOA, ISIWEPO SABABU YA KUACHANA ❤️🙏 1: Ombeni kibali cha Mungu juu ya mahusiano yenu Ee Mungu wetu, tunaweka mahusiano yetu mikononi mwako. Tunaomba utupe kibali chako ili kila hatua tunayopiga iwe chini ya uongozi wako. Tuondolee kila kikwazo kinachoweza kutuzuia kufikia ndoa na utufungulie milango ya baraka na mafanikio. Zaburi 90:17, Mithali 3:5-6 2: Ombeni ulinzi juu ya mahusiano yenu Ee Bwana Yesu, tunaweka mahusiano yetu chini ya ulinzi wako. Linda mioyo yetu dhidi ya usaliti, migogoro, majaribu na kila jambo linaloweza kututenganisha. Tusaidie kudumu katika upendo na kuheshimiana siku zote. Isaya 54:17, Zaburi 121:7-8 3: Ombeni upendo wa kweli udumu Ee Mungu wetu, jaza mioyo yetu upendo wa kweli usio na unafiki. Tusaidie kupendana kwa dhati, kusameheana na kuvumiliana hata tunapopitia changamoto mbalimbali. 1 Wakorintho 13:4-7, Wakolosai 3:14 4: Ombeni amani katika mahusiano yenu Bwana Yesu, tunaomba amani yako itawale katika mahusiano yetu. Ondoa ugomvi, hasira na kutoelewana. Tufundishe kuzungumza kwa upendo na kuheshimiana kila wakati. Wafilipi 4:7, Warumi 12:18 5: Ombeni kushinda maneno mabaya yaliyonenwa juu yenu Ee Mungu wetu, tunafuta kila neno baya lililotamkwa dhidi ya mahusiano yetu. Tunatangaza kuwa hakuna mpango wa adui utakaozuia kusudi lako kutimia katika maisha yetu. Isaya 54:17, Hesabu 23:23 6: Ombeni kuvunja kila kizuizi mbele yenu Bwana, vunja kila kikwazo kinachotuzuia kufikia ndoa. Fungua milango iliyofungwa na utengeneze njia pale ambapo hakuna njia. Isaya 45:2, Luka 1:37 7: Ombeni uaminifu katika mahusiano yenu Ee Mungu wetu, tusaidie kuwa waaminifu kwa maneno na matendo. Ondoa vishawishi vyote vinavyoweza kuharibu uaminifu wetu na kutugawa. Mithali 3:3, Waefeso 4:25 8: Ombeni familia zenu zikubali mahusiano yenu Bwana Yesu, gusa mioyo ya familia zetu na watu wanaotuzunguka ili waone mema yaliyopo katika mahusiano yetu. Tujalie neema na kibali mbele zao. Mithali 16:7, Luka 2:52 9: Ombeni kufika kwenye ndoa yenye baraka Ee Mungu wetu, tunaamini kuwa mahusiano haya hayatabaki hapa bali yataingia kwenye ndoa yenye furaha, amani na baraka. Tusaidie kujiandaa kwa hekima na uvumilivu. Warumi 8:37, Yeremia 29:11 10: Ombeni mapenzi ya Mungu yatimizwe Bwana, tunakabidhi maisha yetu na mahusiano yetu mikononi mwako. Ikiwa haya ni mapenzi yako, yafanikishe na uyafikishe mwisho mwema. Jina lako litukuzwe katika kila hatua ya safari yetu. Hosea 14:1, Zaburi 37:5 Ikiwa umeomba pamoja nami mpaka mwisho, andika neno “Amina” na umtumie mwenza wako maombi haya ili muombe pamoja. ❤️🙏 SIKU 7 ZA KUOMBEA MAHUSIANO NA NDOA 🗓️ Tarehe 1-7/5 (May) Kujiunga tuma neno MAOMBI Tunaombea mahusiano na ndoa zetu. Ndoa yako ikiwa kwenye hali yoyote (furaha au ugomvi) ungana nasi tufunge na kuomba. Unataka kuombea hatima ya mahusiano yako hadi kwenye ndoa? Uwe na mahusiano au huna. Unayo mahitaji yoyote unayotaka kuyaombea na kupokea majibu yako? Jiunge nasi. Sisi kila mwezi tunafunga na kuomba kuanzia tarehe 1 hadi 7. Karibu tuombe pamoja, tuamini pamoja na kushuhudia pamoja yale makuu ambayo Mungu ataenda kuyafanya katika maisha yetu.#TiktokTanzania🇹🇿🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪 #viral #jesuslovesyou

kidotty_bby❤
kidotty_bby❤
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 01 June 2026 16:38:34 GMT
15115
828
57
93

Music

Download

Comments

malume..23
O S C A R 👑 :
daaah mungu atuongoze maana tangu 2019 hadi leo bado tunapendana sana kwa sasa namalizia taratibu za kutoa mahali 🥰
2026-06-03 16:30:04
2
neemjuma6
neemjuma :
Amen 🙏🙏
2026-06-02 06:51:59
1
nancy.sengasu5
Nancy Sengasu :
ameen
2026-06-04 11:33:29
0
miss.feb5
miss feb🦋 :
Amen
2026-06-04 09:48:07
0
marrymushi55
merry :
amen
2026-06-02 04:53:19
0
jahny.2007
jahny 2007 :
amen
2026-06-01 21:12:44
0
brigitqueen
brigitaqeen :
Amen 🙏
2026-06-02 06:33:56
0
elicemabele1
Licy😍 :
Amen
2026-06-02 07:59:25
0
veronica.swai1
Veronica Swai :
amen🤲🙏
2026-06-02 07:03:41
0
phinaonexy
phina onexy :
Amen amen
2026-06-01 21:19:12
0
bhujuuwangu7
❤️ ❤️ :
ameen 🙏🏻🙏🏻
2026-06-02 04:16:49
0
lavidah0
vidah :
Amen
2026-06-01 20:45:26
0
anniendwete
officialannie1 :
amen
2026-06-03 17:29:58
0
its.leen58
💞it’s leen🌸💕 :
Amen 🙏
2026-06-03 16:31:33
0
missnanah0
Nanah :
Maombi
2026-06-03 19:21:51
0
happygiven......1
Happy@given❤🤍 :
Ameni 🙏
2026-06-03 22:25:03
0
jahny.2007
jahny 2007 :
amen🙏🙏🙏🙏
2026-06-01 21:14:41
0
missnanah0
Nanah :
Maombii
2026-06-03 19:21:58
0
user68878380200744
Vann cute❤️ :
Ameni🙏
2026-06-04 19:58:33
0
roseadam03
roseadam03 :
Amen🙏🙏🙏 Mungu nitangulie kwenye uu uhusiano mpya niliyo aanza nikafikie hatu ya kuingia kwenye ndoa na Justin
2026-06-04 03:39:37
0
mane_beuty
mane :
Amen
2026-06-04 11:34:10
0
_.benitho
𝓑𝓮𝓷𝓲𝓽𝓱𝓸 :
Amen🙏🏻🙏🏻
2026-06-04 15:21:22
0
salvina7070
salvina :
amen
2026-06-04 06:36:11
0
vee23cute
✨Vee🦋 :
Amen
2026-06-04 06:20:30
0
emmy29093
emmy❤️💕 :
amenn🙏
2026-06-02 08:29:14
0
To see more videos from user @kidotty_bby, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About